https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
3 9 4 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Mungu Wetu Asimame! (muendelezo)
Mungu Wetu Asimame! katika vitongoji vilivyokumbwa na vurugu na hofu! Mungu Wetu Asimame! katika nyumba za ibada na makusanyiko yaliyotishwa na kuzingirwa! Mungu Wetu Asimame! kwa kumiminwa kwa Roho wake Mtakatifu ambako kutasababisha mwamko wa kiroho na maendeleo makubwa ya Ufalme miongoni mwa watu maskini zaidi katika miji ya Marekani. Tunatoa kwenu wito wa maombi endelevu: je, hutaungana nasi katika kumlilia Mungu mchana na usiku kwa niaba ya majiji na wakazi wake, kutoka New York hadi Los Angeles, na wale wote wanaohitaji kusikia juu ya upendo wa Mungu unaookoa katika Kristo? Tunatoa kwenu wito wa dhati wa maombi endelevu: je, unaelewa jinsi mchango wako unavyoweza kuwa muhimu ikiwa tu utajitoa katika maombi yasiyokoma, yasiyotikisika, yaliyojaa imani kwa Mungu kwa niaba ya moja ya maeneo muhimu ya kimisheni magumu zaidi duniani? Tunatoa kwenu wito wa dhati wa maombi endelevu : je, utamruhusu Mungu, Roho Mtakatifu akufundishe kuwa shujaa katika ulimwengu wa kiroho, anayemlingana Mungu kwa njia ya maombezi kwa niaba ya Kanisa ambalo linasinzia na linahitaji kuamshwa, na ulimwengu unaokufa na unaohitaji kusikia juu ya utawala wa Mungu uletao uzima na utawala wenye nguvu uliopatikana kwa ajili yetu kupitia Yesu Kristo na kifo chake msalabani? Tukutane kwa mapatano matakatifu, wawili au watatu (Mt. 18:20) au ukumbi mzima wa waombaji (2 Nya. 20) ili kumtafuta Bwana na kuisihi neema ya Bwana kwa niaba ya miji. Na tufanye hivyo katika vyumba vyetu vya maombi binafsi, vikundi vyetu vya seli na katika maeneo ya kujifunza ya vikundi vidogo, katika makusanyiko yetu na ibada za kanisa, katika mikutano na makongamano yetu ya maombi, katika matamasha yetu ya mikesha ya maombi, mifungo, majumbani, mashuleni – popote ambapo Bwana anaweka mioyoni mwetu kumsihi atembelee miji ya dunia, na mji wetu. Ebu tujitoe kumlingana Mungu hadi atakapotutembelea. Tukifanya hivyo, miji ya Marekani (na pengine, ya dunia nzima) haitabaki kamwe kama ilivyo. Ni Mungu Pekee Anayeweza Kuwafanya Upya Watu Wake. Ni Mungu Pekee Anayeweza Kuokoa Majiji.
Made with FlippingBook Annual report maker