https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

5 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Katika sehemu hii tumeangazia vipengele vya taswira ya Utume kama Utimilifu wa Ahadi ya Mungu ambayo inazungumzia utendaji wa Mungu kama utimilifu wa ahadi yake kwa Ibrahimu na Daudi. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu kwa habari ya Mzao ambaye angekuwa Baraka kwa wazao wake, na kupitia kwao kwa jamaa zote za dunia, ilithibitishwa kwa Isaka na Yakobo, na kwa kabila la Yuda. Ahadi hiyo ya agano kwa habari ya Mzao ambaye angekuwa Baraka kwa mataifa iliunganishwa pia na rehema ambazo Mungu alimpa Daudi katika ahadi ya mrithi wa kudumu kwenye kiti chake cha ufalme. Sasa, katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ahadi ya agano la Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa. Umisheni unatangaza maisha haya mapya kupitia uaminifu wa Mungu kwa agano lake. Ni muhimu kwamba uweze kutoa muhtasari huu mfupi katika kuhubiri na kufundisha kwako, kwa hiyo pitia mambo muhimu hapa kupitia maswali yaliyo hapa chini. 1. Fafanua kwa ufupi taswira ya utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu . Ni kwa njia gani mada hii inategemea ufahamu wa kibiblia wa agano? Agano ni nini? 2. Maagano yanapatikana mara ngapi katika Maandiko, na ni baadhi ya sifa gani zinazofanana za maagano yote katika Biblia? Utamaduni wa Waisraeli ulimwonaje mvunja agano? Eleza masharti na manufaa yanayohusiana na maagano katika Biblia, na jinsi gani yalitiwa muhuri, kushuhudiwa, na kuthibitishwa. 3. Aina gani ya agano pengine ndio ya kawaida katika Biblia? Orodhesha maagano mawili makuu zaidi ambayo Mungu alifanya ambayo yanaweza kuonekana katika historia yote ya Israeli. 4. Taja vipengele mahususi vya agano la Ibrahimu – masharti yake na faida zilizoahidiwa zilikuwa zipi? Ahadi hiyo iliainishwaje kwa kabila la Yuda, na tamko hilo lilitolewa lini? 5. Ahadi ya Mungu kwa Daudi iliyorekodiwa katika 2 Samweli 7 inahusianaje na ahadi kwa Ibrahimu ambayo ilifafanuliwa kupitia Yuda? Ni ahadi gani mahususi ambazo Mungu alimpa Daudi kuhusu Uzao wa kifalme— angefanya nini, na Mungu angemfanyia nini? 6. Ahadi za Mungu kwa Abrahamu na Daudi zinatimizwaje katika Yesu wa Nazareti? Maisha, kifo, ufufuo, na kupaa kwake kunatoaje uthibitisho wa wazi kwamba ahadi ya Mungu kwa Abrahamu na Daudi imetimizwa sasa?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

1

Made with FlippingBook Annual report maker