https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 5 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
7. Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba utume unathibitisha na kutangaza uaminifu wa Mungu kwa agano lake kupitia Yesu kama utimilifu wa ahadi yake kwa Abrahamu na Daudi katika enzi ya sasa? Je, kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi kwa kutii Agizo Kuu kunawakilishaje utimilifu wa ahadi kwa watu wa mataifa? (rej. Gal. 3 na Rum. 16:25-27, Kol. 1:25-29, na Efe. 3:1-10). 8. Kwa nini mada hii ya ahadi na utimilifu ndio kiini cha kazi ya umisheni? Je, inawezekana kutangaza Injili kwa uwazi katika utume bila kuzungumzia utimilifu wa ahadi kwa Ibrahimu na Daudi kupita Yesu Kristo? Ikiwa jibu ni ndiyo au hapana, eleza kwa nini. Somo hili linazingatia mada mbili tofauti za utume ambazo zinatuwezesha kupata «picha kubwa» ya kile ambacho Mungu amekuwa akifanya ulimwenguni, na jinsi kinavyohusiana na kazi yetu ya kuendeleza utawala wa ufalme wake. Kauli zifuatazo zinawakilisha dhana kuu zinazoshughulikiwa katika somo, na zinapaswa kupitiwa tena kwa faida ya msisitizo na uelewa. (Daima kumbuka, tendo la kurudia dhana zile zile tena na tena ni muhimu katika kuwezesha wanafunzi kuzishika vyema, rej. Yos. 1:8; Flp. 3:1). ³ Neno “ prolegomena ” linamaanisha “neno la kwanza,” na p rolegomena juu ya utume lazima ianze na mtazamo wa kibiblia wa ulimwengu juu ya Mungu na kazi yake duniani kupitia Yesu wa Nazareti. ³ Utume unaweza kufafanuliwa kama “tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kazi yake katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa makundi yote ya watu.” ³ Uelewa wa kibiblia wa utume una vipengele fulani ambavyo vinaweza kubainishwa kutokana na usomaji wa Maandiko yenyewe. Utume lazima ujengwe juu ya msingi wa ufahamu sahihi wa Mungu na makusudi yake kwa ulimwengu, kuhusianisha maelezo yote ya kihistoria katika mada moja. Mtazamo wa kibiblia wa utume, pia, lazima ujikite katika Maandiko yenyewe, ukiwa umejengwa katika Yesu Kristo na kazi yake, na kuchukua kwa uzito njia ya kibiblia ya kujadili utume kupitia taswira, picha, na hadithi. ³ Katika Maandiko tunaweza kupata taswira nne au picha nne za kitheolojia za utume, yaani, utume kama Tamthilia ya Nyakati Zote (Mungu kama mhusika mkuu katika hadithi kuu ya wakati wote); utume kama utimilifu
1
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook Annual report maker