https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

5 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

wa ahadi ya Mungu (Mungu akitimiza ahadi yake ya agano kupitia Yesu Kristo), utume kama Mapenzi ya Enzi (Mungu kama Bwana-arusi wa jamii yake mpya ya wanadamu waliokombolewa); na Utume kama Vita vya Milki (Mungu kama Shujaa akianzisha tena utawala wake juu ya ulimwengu). ³ Vipengele vya taswira ya Tamthilia ya Nyakati Zote vinaweza kueleweka katika msingi wa awamu kuu za kusudi la Mungu linaloendelea kufunuliwa, tangu Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati . Kabla ya Wakati huangazia uwepo wa Mungu kabla ya mwanzo na kusudi lake, siri ya kuasi na uasi wa mamlaka; Mwanzo wa Wakati ni pamoja na uumbaji wa ulimwengu na wanadamu, anguko na laana, protoevangelium [yaani tamko la kwanza la Injili], mwisho wa Edeni, kifo, na ishara za kwanza za neema. Kufunuliwa kwa Wakati ni pamoja na ahadi kwa Ibrahimu, Kutoka, Kutekwa kwa Nchi, Jiji-Hekalu-Kiti cha Enzi, Utumwa na Uhamisho, na Kurudi kwa Mabaki. ³ Kusudi la Mungu linaloendelea kujifunua kuelekea katika awamu ya Utimilifu wa Wakati ni pamoja na Kristo kuvaa mwili, kufunuliwa kwa Ufalme katika Yesu, mateso, kifo, ufufuo, na kupaa kwa Kristo. Nyakati za Mwisho ni pamoja na kushuka kwa Roho Mtakatifu, kuanzishwa kwa Kanisa, kujumuishwa kwa Mataifa, na enzi ya utume wa ulimwengu. ³ Awamu ya Ukamilifu wa Wakati inajumuisha mwisho wa uinjilishaji wa ulimwengu, uasi wa Kanisa, Dhiki Kuu, Parousia , utawala wa Kristo duniani, Kiti Kikubwa cha Enzi Cheupe, Ziwa la Moto, na Kristo kukabidhi Ufalme kwa Mungu Baba. Hatimaye, awamu ya Baada ya Wakati inajumuisha mbingu mpya na nchi mpya, kushuka kwa Yerusalemu Mpya, nyakati za kuburudishwa, na kuingizwa kwa Enzi Ijayo. ³ Taswira ya utume kama Tamthilia ya Nyakati Zote inaeleza jinsi kusudi kuu la Mungu linavyoweka msingi wa historia yote ya mwanadamu, Mungu kama mhusika mkuu katika awamu za tamthilia ya kiungu zinazoendelea kujifunua, utume kama kurejesha kile kilichopotea mwanzoni mwa wakati, na kazi ya kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi kama sehemu yetu katika kutimiza jukumu letu katika muswada (script) wa Mwenyezi Mungu . ³ Mojawapo ya motifu (mada) kuu nne zinazoelezea utume katika Maandiko ni motifu ya utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu . Kwa maana ya kibiblia, agano ni mapatano au mkataba kati ya pande mbili, iwe watu binafsi, makabila, au mataifa; pamoja na kuwa na wajibu wa kutimiza masharti

1

Made with FlippingBook Annual report maker