https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 5 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

ya mkataba huo, na faida na manufaa kama matokeo ya kutimizwa kwa masharti hayo. ³ Maagano ya Kibiblia ni mengi, na yana sifa zinazofanana, ikijumuisha jinsi maagano na/au mikataba ilivyosimamiwa na shahidi na kubeba madhara makubwa endapo wahusika wangevunja masharti ya maagano au mikataba hiyo (kuvunja mkataba kulichukuliwa kuwa ni uovu mkubwa sana kimaadili). Maagano yalitiwa muhuri na kutolewa ushahidi kwa kutoa zawadi, kula chakula, na mara nyingi yalijumuisha kuweka mawe ya ukumbusho. Yalithibitishwa kwa kula kiapo na kutoa dhabihu. ³ Pengine aina ya kawaida ya agano la kibiblia ilikuwa sherehe ya ndoa, na maagano mengine maarufu yanaweza kuonekana katika historia yote ya Israeli, kwa mfano, agano la Mungu na Nuhu, na agano lake na wana wa Israeli Sinai. Maagano ya Mungu, yawe yenye masharti au yasiyo na masharti, yote yanazungumzia mkataba mzito kati ya Mungu na watu binafsi au na watu wake wateule. ³ Taswira ya utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu inaweza kufuatiliwa kutoka agano la Mungu alilofanya na Ibrahimu, pamoja na sharti lake la kwamba aondoke katika nchi yake na jamaa yake na kwenda katika nchi aliyoichagua Mungu mwenyewe, pamoja na baraka inayoambatana na sharti hilo kwamba Mungu angemfanya kuwa taifa kubwa, angembariki na kulikuza jina lake, kuwabariki wambarikio na kuwalaani wamlaanio, na kuzibariki jamaa zote za dunia kupitia yeye. ³ Agano la Mungu na Abrahamu la kumleta Mzao ambaye angekuwa baraka kwa mataifa lilihuishwa na kuthibitishwa katika wazao wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, na baadaye likafafanuliwa kwa ajili ya Yuda, kabila ambalo Masihi wa Mungu angetokea. Miongoni mwa familia za Yuda, nyumba ya Daudi ilichaguliwa na Mungu kuwa nyumba ambayo Uzao wa kifalme wa baraka za Abrahamu ungetokea. Mrithi wa Daudi angetawala milele juu ya nyumba ya Israeli na kuwa baraka kwa mataifa. ³ Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi ilitimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ambaye anawakilisha Mzao wa Abrahamu na mwana wa Daudi ambaye kupitia yeye utawala wa Mungu ungesimamishwa. Kupitia maisha, kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu, ahadi ya agano la Mungu inatimizwa. ³ Utume ni uthibitisho na utangazaji wa Habari Njema hii kuhusu uaminifu wa agano la Mungu kupia Yesu Kristo, na Agizo Kuu ni jukumu la kutangaza na kufundisha ahadi hii iliyotimizwa kwa ajili ya wanadamu wote, kuanzia Yerusalemu, hadi miisho kabisa ya dunia.

1

Made with FlippingBook Annual report maker