https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
5 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
³ Kiini cha kazi ya umishenari ni kwamba kupitia Yesu wa Nazareti, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa na sasa, kwa njia ya kutangaza Injili, ahadi ya uzima wa milele inatolewa bure kwa mataifa kwa njia ya kuhubiriwa kwa Neno la msalaba.
Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu mada na taswira zilizoshughulikiwa katika somo hili. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia maarifa ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, umekuwa na uzoefu gani katika kanisa lako kuhusu suala la “umisheni”? mtazamo kuhusu umisheni umekuwa wa aina gani katika uzoefu wako? * Je, umewahi kukutana na wamishenari wowote? Walikuwa wakihudumu wapi? Ni aina gani za masuala, mada na dhana ambazo walisisitiza ulipopata muda pamoja nao? Kwa kuzingatia uzoefu wako, ni mambo gani uliyoyaona kuhusu kazi ambayo wamishenari wanaifanya na nia zinazowasukuma kufanya kazi zao? * Kwa nini unafikiri ni muhimu kuanza majadiliano kuhusu umisheni na kile ambacho Maandiko yanafundisha, na si kwa uzoefu na historia za wamishenari mbalimbali katika historia? Elezea. * Je, umewahi kufikiria kuingia katika utumishi wa kudumu kama mmishenari? Ni mambo gani ambayo yalikufanya ufikirie umeshenari kama kazi ya kuifanya katika maisha yako? * Je, ni kwa kiasi gani unaweza kueleza kutoka katika kumbukumbu yako (bila kusoma vitabu) hadithi ya Mungu kama ilivyoonyeshwa katika muhtasari wa tangu Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati ? Kwa nini muhtasari kama huo unasaidia kuelezea kwa ufupi umisheni kama tangazo la sasa la hadithi ya Mungu, yaani, fursa ambayo ametoa ya wokovu na ukombozi katika Yesu Kristo na kazi yake? * Kamilisha sentensi ifuatayo: “Jambo moja linalonisukuma na kunipa changamoto zaidi katika kujadili umisheni kulingana na hadithi ya Mungu ya tangu Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati ni .…… * Bila kutumia vitabu au Biblia, elezea ahadi ya agano la Mungu kuanzia Uzao wa mwanamke katika Mwanzo 3:15 hadi utimilifu wa agano katika Yesu Kristo. Jumuisha ahadi ya Mungu katika bustani, kwa Shemu, kwa
Kutendea Kazi Somo na Matekeo yake kwa Wanafunzi
1
Made with FlippingBook Annual report maker