https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 5 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwa Yuda, kwa Daudi, na hatimaye kwa Kristo. (Umepatia kwa kiasi gani? Je, umeweza kujumuisha marejeo ya mistari ya Biblia husika kwa kila kipengele?) * Je, una mwelekeo wa kuona kazi ya Mungu kulingana na picha kubwa, au unapotea katika maelezo ya kila siku ya kutembea kwako na Mungu? Eleza. Tabia hii ya kuona mbali au kutokuona mbali ilianzia wapi katika kutembea kwako na Kristo? * Kwa nini itakuwa muhimu kila wakati kuona kile kinachoendelea katika maisha yetu katika muktadha wa kile ambacho Mungu amekuwa akifanya kwa karne nyingi ? Ni kwa jinsi gani maono na mkazo wa umisheni vinaweza kutupatia mtazamo kama huu? * Kamilisha sentensi ifuatayo: “Jambo moja ambalo lingenisaidia kupanua mtazamo wangu wa kile ambacho Mungu anafanya ulimwenguni leo ni .... Katika kitabu chake cha kuvutia chenye kichwa: “ Reconnecting God’s Story to Ministry: Cross-cultural Storytelling At Home and Abroad” (Kuunganisha Upya Hadithi ya Mungu na Huduma: Kusimulia Hadithi katika Tamaduni Mbalimbali Ndani na Nje ya Nchi), Tom Steffen anatoa msisitizo mkubwa kuhusu ulazima wa kurejea kwenye masimulizi na kusimulia hadithi katika uinjilisti na uanafunzi (ufuasi). Anabainisha kile anachokiita “nchi za hadithi” miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu, na anasema kwamba utume, yaani, kazi ya Kanisa kutangaza Habari Njema kwa waliopotea miongoni mwa watu wasioenda kanisani ambao hawajafikiwa, ni kuwa mwaminifu kwa hadithi ya Mungu huku tukiwa wazi kwa hadithi za wengine na hadithi zetu wenyewe. “Ili kufikia wale wanaoishi ndani ya nchi-ya-hadithi mahususi, msimuliaji wa hadithi lazima atambue si tu simulizi za Biblia, bali pia za kikundi cha watu husika, na hasa, za kwake mwenyewe.” (Tom Steffen, Reconnecting God’s Story to Ministry . La Habra, CA: Centre for Organizational and Ministry Development , 1996, uk. 15). Anaamini kwamba kila moja ya “nchi-za hadithi” hizi ni ya msingi na muhimu kwa kufanya umisheni katika ulimwengu wa leo. Je, unafikiri nini kuhusu maoni yake ya jumla, kwamba kiini cha utume na huduma ni kujifunza kusimulia na kusikia hadithi za wengine na za kwetu wenyewe, huku tukiwa makini kila mara kuunganisha haya yote mawili na hadithi moja ya msingi, hadithi ya Mungu katika Maandiko kuhusu Yesu wa Nazareti na wokovu katika yeye? Utume kama Kusimulia Hadithi – Kielelezo kwa ajili ya Huduma

1

MIFANO

1

Made with FlippingBook Annual report maker