https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
6 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Ni Ubinafsishaji Uliopitiliza wa Ahadi za Mungu?
Kutokana na msisitizo mkubwa juu ya ubinafsi na masuala binafsi leo, Ukristo kwa wengi umekuwa jambo la kibinafsi kabisa. Ahadi zote na matamko yote ya Biblia yanaeleweka na kuchukuliwa katika mitazamo ya kimaisha ya kibinafsi kupita kiasi, na wengi wamefikia hatua ya kuona maisha yote ya Kikristo kama «uhusiano kati yangu na Mungu.» Mwenendo huu unaonyeshwa katika mambo kadhaa tofauti: mwelekeo wa muziki wa kuabudu ambao unalenga kabisa hali ya kihisia na kisaikolojia ya mwabudu, kuenea kwa mfumo wa makanisa makubwa ambayo yanasisitiza utatuzi wa matatizo ya mtu binafsi, mlipuko wa huduma za kanisa zinazolenga kusaidia watu binafsi kushinda masuala na changamoto zao binafsi, na kuhama kwa watu wengi kisaikolojia kutoka Kanisani. Wengi leo wamepuuza ushirika wa kanisa, wanaona kuhudhuria kanisani kama si lazima au kunafaa tu ikiwa linashughulikia mahitaji fulani ya mtu binafsi na/au familia. Makanisa yameitikia mienendo hii, na kuwa zaidi kama maduka ya idara fulani za kidini kuliko makusanyiko yenye uhai. Je, unafanya nini kuhusu «ubinafsishaji» wa maisha ya Kikristo? Je, ahadi ya Mungu kwa ajili ya Mwokozi wa ulimwengu inajiruhusu kubinafsishwa kwa urahisi, au je, mienendo yetu ya sasa ya Ukristo wa watu binafsi inawakilisha kuondoka kwetu kutoka kwenye msisitizo wa «watu wa Mungu» katika Agano la Kale na Agano Jipya? Je, ni lugha gani yenye ufanisi zaidi ya kuwasilisha Injili kwa utamaduni uliopotea leo? Guilford Dudley III anasema kuwa lugha ya hekaya ndiyo lugha ambayo lazima tuirejeshe. Dudley hatumii neno hili kumaanisha simulizi za miungu zisizo na ukweli wa kihistoria, bali aina ya hadithi za maisha na ulimwengu kwa ujumla ambazo zinathubutu kuelezea ujumla wa maisha na ulimwengu katika tamthilia yake. “Mtu mmoja mashuhuri katika Uprotestanti wa Marekani amewaambia waandishi wa habari mara kwa mara: ‘Kwa kiwango hiki cha kuporomoka kwa Ukristo, ni muhimu kusafiri ukiwa mwepesi. Ninataka kuondoa mizigo mingi ya kitheolojia kadri niwezavyo.’ Maneno hayo ya kichochezi yanaonyesha mtazamo unaoongezeka ndani ya makanisa ya Kiprotestanti katika nchi hii. Katika jitihada zao za kuzuia kile kinachoitwa “kuporomoka kwa Ukristo,” makanisa mengi yanaonyesha utayari wa kutisha wa kutupilia mbali mawazo na lugha zote ambazo haziendani moja kwa moja na kile ambacho wamekiona kuwa kanuni za maisha ya usasa. Lugha ambayo wameiacha kwa hiari na kirahisi zaidi ni lugha ya mifano, ishara na hadithi. Maamuzi hayo yamewaweka katika njia ya hatari, na kuwaacha wakiwa mbali zaidi na mifumo halisi ya mawasiliano ya kweli na tamaduni zetu. Wanatathmini vibaya utamaduni, na kuwekea mipaka maana ya Kufufuliwa kwa Hadithi ya Kikristo
2
1
3
Made with FlippingBook Annual report maker