https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 6 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

usasa na lugha ya Injili. Kitabu hiki ni uchunguzi wa kutaka kuonyesha ni utajiri kiasi gani tunaupoteza tunapoacha kutumia lugha ya hadithi ambayo makanisa yanaharakisha kuikana, na kwa hakika jinsi lugha hiyo inavyokataa kupotea katika moyo wa utamaduni wetu. Kwa sababu, ingawa lugha ya hadithi inaonekana kutengwa mbali na lugha rasmi ya kanisa, imejitokeza tena katika kazi mashuhuri za sanaa ya fasihi inayotoa ushuhuda wa nguvu zake zenye kuhuisha” (Guilford Dudley III, The Recovery of Christian Myth . Eugene, OR: Wipf naStock Publishers, 2004, uk. 13). Ingawa iliandikwa mwishoni mwa miaka ya 60, kazi ya Dudley kwa namna ya kinabii inasisitiza kwamba tumeacha «lugha ya asili» ya Ukristo, yaani lugha ya picha, ishara, hadithi, na mifano na kukumbatia maelezo ya kisayansi kuhusu uwezekano wa imani. Je, una maoni gani kuhusu madai ya Dudley, na kama ni kweli, unafikiri nini kitatokea kwa juhudi za umisheni wa Kikristo ikiwa tutatumia mbinu za kimantiki [kisayansi] na uzoefu wetu katika kuitangaza imani yetu? Utume ni tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kazi yake katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa makundi yote ya watu . Ukitazamwa kama tamthilia na hadithi ya Mungu, kutoka Kabla ya Wakati hadi Baada ya Wakati , tunaweza kuanza kuona jinsi ambavyo katika hadithi ya utume, Mungu wa Utatu anatenda kazi kama Mungu Mwenye Enzi Kuu , akitenda kazi katika mambo yote kwa utukufu wake na manufaa yetu. Taswira ya Utume kama Utimilifu wa ahadi ya Mungu inaelezea kazi ya Mungu kama kutimiza ahadi yake kama Mungu mwaminifu kwa agano lake kwa Ibrahimu na Daudi. Ikijengwa juu ya jukumu la agano la kibiblia katika Maandiko, mada hii inaanza na ahadi ya Mungu ya agano kwa Ibrahimu, iliyothibitishwa kwa wanawe na mababa au taifa la Israeli, na baadaye kuhusishwa na kabila la Yuda. Ahadi hiyo ya agano kwa ajili ya Mzao ambaye angekuwa baraka kwamataifa ilikuzwa na kufafanuliwa katika ahadi kwa Daudi ya kuwa na mrithi wa kudumu kwenye kiti chake cha ufalme. Sasa katika wakati huu na katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi imetimizwa. Vivyo hivyo, katika enzi hii kwa njia ya kutangaza Injili kupitia utume, ahadi ya maisha mapya inatolewa kwa mataifa kwa njia ya mahubiri ya Neno la msalaba.

1

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Ikiwa ungependa kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo ya somo hili la Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Kwanza , unaweza kutaka kusoma vitabu hivi:

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook Annual report maker