https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
6 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Bartholomew, Craig G., and Michael W. Goheen. The Drama of Scripture: Finding Our Place in the Biblical Story . Grand Rapids: Baker Academic Books, 2004. Goldsworthy, Graeme. According to Plan: The Unfolding Revelation of God in the Bible . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2002. Roberts, Vaughan. God’s Big Picture: Tracing the Story-Line of the Bible. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2003. -----.Life’s Big Questions: Six Major Themes Traced Through the Bible. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2005. Uwezo wako wa kufanya mada hizi kuwa wazi kwa wengine utategemea uwezo wako wa kutumia mada na mitazamo ya Maandiko katika maisha na huduma yako mwenyewe. Tamthilia ya Maandiko, maono ya ahadi ya Mungu na utimilifu wake katika Kristo, ni kwa ajili yako kwanza, kabla hujafikiria kuhusu kueleza, kutangaza, au kuwaalika wengine kupata ukweli wake na nguvu zake zinazohuisha. Tafakari juu ya kweli hizi, na umwombe Roho Mtakatifu akuelekeze kwenye fursa ya kuhusianisha kweli hizi na huduma kwa vitendo, ambayo utafikiria na kuombea katika wiki hii yote ijayo. Mungu hataki ufikirie tu kuhusu tamthilia yake; badala yake, anataka uiishi . Vivyo hivyo, Mungu hataki tu usome juu ya ahadi na utimilifu wake katika Yesu; anataka uzikiri kwa moyo wako wote. Mwombe Roho Mtakatifu aweze kutumia kweli hizi na mitazamo hii katika maisha yako, na ujitoe kwake ili akuongoze unapotafakari kweli hizi wiki hii. Omba kwa Bwana akupe nguvu za kuelewa na kutumia kweli hizi katika maisha yako mwenyewe, na katika maisha ya wanafunzi wenzako. Kumbuka, lengo ni kwamba tupate kubidishwa na kushawishiwa kwa kina kabisa na hadithi hii, na kwamba tujione kama sehemu ya ahadi iliyotimizwa katika Kristo. Omba kwa Bwana kwamba kweli hizi zichukue umuhimu mpya katika maisha na huduma yako, na kwamba Roho akusaidie kuona Biblia kama hadithi moja inayoendelea kujifunua, hadithi ya kazi ya Mungu ulimwenguni, na nafasi yetu kama wahusika katika hadithi hiyo. Omba ili Bwana akusaidie kupata maana kubwa zaidi ya umoja wa Biblia, ya uwezo wa Agano la Kale kama maandalizi kwa ajili ya kazi ya Kristo, na utume kama kielelezo cha umoja kati ya kile Mungu alichoahidi katika Agano la Kale na kile alichotimiza katika Agano Jipya kwa njia ya Yesu Kristo. Zaidi ya yote, mwombe Bwana afanye kweli hizi kuwa hai maishani mwako unapotafuta nia ya Mungu kupitia kujifunza kwako na kutumia Maandiko.
1
Kuhusianisha Somo na Huduma
Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook Annual report maker