https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 6 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
MAZOEZI
Waebrania 6:17-18
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya usomjai ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Ili kuhakikisha kwamba kujifunza kwako moduli hii kunaleta matokeo mazuri, utahitaji kutenga muda kwa ajili ya kazi zako zijazo, ikiwa ni pamoja na muda wa kupitia maeneo ya kusoma ya wiki hii katika kujiandaa kwa ajili ya kazi ya usomaji. Katika kipindi kijacho cha darasa, utafanya jaribio kuhusiana na maudhui ya somo la wiki hii (yaliyomo kwenye video). Hakikisha kwamba unatumia muda mzuri kupitia vitabu na madaftari yako, hasa ukikazia fikira mawazo makuu ya somo. Pia, tafadhali kamilisha maeneo yako usomaji uliyogawiwa, na uandike muhtasari wa usomaji wako. Muhtasari wako usizidi fungu moja au mawili kwa kila eneo la usomaji, na unachopaswa kuandika ni mwitikio wako na maoni yako bora kuhusu kile ulichoona kuwa jambo kuu katika kila eneo husika la usomaji. Usijali sana juu ya kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumzwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali leta muhtasari huo darasani wiki ijayo. (ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Katika somo hili tuligundua “ prolegomena ” kwa ajili ya umisheni: ufafanuzi mfupi kwamba utume ni tangazo la fursa ya wokovu na ukombozi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo na kazi yake katika uwezo wa Roho Mtakatifu kwa makundi yote ya watu . Tuliona jinsi taswira mbili, utume kama Tamthilia ya Nyakati Zote na utume kama utimilifu wa ahadi ya Mungu zinavyoweza kutuwezesha kuona kazi ya Mungu ulimwenguni kama hadithi moja inayoendelea kujifunua. Mungu Mwenyezi, Mungu mwaminifu kwa agano lake, ametimiza ahadi yake kupitia Yesu wa Nazareti, ambaye anawakilisha utimilifu wa mpango na kusudi la Mungu la kukomboa uumbaji wake. Utume ni utimilifu wa kusudi hilo kuu kwa ajili ya utukufu wake na wokovu wa mataifa. Katika somo letu linalofuata, tutaendelea kuchunguza taswira za utume katika Maandiko, tukitazama kazi ya Mungu ya uokozi kama Mapenzi ya Kiungu na Vita vya Milki . Kuhusiana na mapenzi ya kiungu, Bwana ameamua kuwatoa watu katika ulimwengu ili wawe milki yake mwenyewe, na sasa kupitia Yesu Kristo na Kanisa lake, mada ya mapenzi inapata utimilifu wake mkubwa zaidi. Kuhusiana na mada ya vita, Mungu ameamua kusimamisha tena utawala wa ufalme wake kupitia Yesu wa Nazareti. Tangu Anguko, Mungu amechukua nafasi ya Shujaa ili kurudisha ulimwengu chini ya utawala wake. Katika Yesu wa Nazareti, Mungu anathibitisha tena haki yake ya kutawala ulimwengu wake, na utume ni udhihirisho na utangazaji wa mamlaka hiyo ya ufalme, ambayo sasa imekuja katika Kristo.
Kazi Nyingine
1
Kuelekea Somo Linalofuata
Made with FlippingBook Annual report maker