https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 6 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Pili

SOMO LA 2

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake kama mojawapo ya sababu kuu za utume katika Maandiko, yaani, azimio la Mungu la kuvuta watu kutoka ulimwenguni ili wawe milki yake mwenyewe, milki iliyotimizwa na kukamilishwa katika upendo wa Yesu kwa Kanisa lake. • Kuelezea wazo la bwana-arusi na bibi-arusi katika Agano la Kale, ikijumuisha uhusiano wake na wazo la furaha na shangwe katika Maandiko, matumizi yake kama taswira ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake (kama inavyoonekana katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora), na jinsi uhusiano wa Mungu na watu wake ulivyokua, kutoka asili ya kusikitisha ya taifa la Israeli hadi hukumu na uhamisho wao kwa kutokuwa mwaminifu kwa Mungu. • Kuelezea kwa kina kurudi kwa mabaki katika nchi, kutokana na amri ya Koreshi kwa mabaki kurudi, kuingia kwao tena kihalisi katika nchi chini ya Ezra, Zerubabeli, na Nehemia, na ahadi ya Mungu ya agano jipya, si kwa msingi wa utii na uaminifu wao bali kuandika sheria yake mioyoni mwao na kuwapa roho mpya. Hatimaye, watu wake wangerudishwa kwa Mungu, ambaye angecheza na kushangilia juu ya watu wake kama bwana arusi juu ya bibi-arusi. • Kufuatilia baadhi ya madokezo makuu ya ahadi ya agano jipya iliyotolewa katika Agano la Kale, ikijumuisha agano la Ibrahimu na matarajio yake ya kujumuishwa kwa Wamataifa, na kuonyesha jinsi ambavyo kwa njia ya Yesu Kristo, taswira ya bibi-arusi inavyopanuliwa na kukamilishwa. Yesu anakuwa chanzo na uzima wa Kanisa, bibi-arusi wake mpya, na Yohana Mbatizaji akiwa rafiki wa bwana-arusi. • Kuonyesha jinsi wazo la watu wa Mungu lilivyofunuliwa kupitia kufunuliwa kwa siri kupitia mitume na manabii, kwamba Mataifa ni warithi pamoja na Wayahudi katika ahadi ya agano jipya la Mungu, na kupitia hilo, wanakaribishwa kama washiriki wa jamii mpya ya watu wa Mungu na bibi arusi wa Kristo.

Malengo ya Somo

2

Made with FlippingBook Annual report maker