https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

6 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

• Kuorodhesha mambo makuu ya mafundisho yanayohusiana na kujumuishwa kwa watu wa mataifa kama bibi-arusi wa Kristo, ikiwa ni pamoja na kukaribishwa kwao kwa njia ya imani, azimio la suala hilo kwenye Baraza la Yerusalemu, nguvu ya damu ya Kristo kuwajumuisha katika agano, namna ambavyo kiini cha huduma ya kitume ni kuwatayarisha watu wa Mungu kama bibi-arusi, ambaye Kristo atampokea akija bila mawaa machoni pake. • Kueleza jinsi mapenzi ya kiungu yatakavyokamilishwa kwa kushuka kwa Yerusalemu Mpya kutoka mbinguni, makao ya Mungu na watu wake, ambao watajitambulisha kikamilifu na Kristo, bwana-arusi, kwa kubadilishwa na kufanana na yeye, warithi pamoja naye, wakiwa katika uwepo wake milele kama watawala pamoja naye. • Kuonyesha madokezo makuu ya mapenzi ya kiungu, ikijumuisha nia ya Mungu ya kuvuta watu kutoka kwa mataifa yote kwa ajili yake, taswira inayojumuisha Wayahudi na watu wa mataifa, na kwa sababu hiyo utume ni ushuhuda kwamba Mungu anawavuta washiriki wa jamii ya ufalme wake kutoka kwa Wayahudi na kwa mataifa, ambao wataishi naye milele. • Kuelezea taswira ya Utume kama Vita vya Milki , ambayo labda ndiyo taswira ya utume yenye nguvu zaidi katika Maandiko, tangazo la utawala wa ufalme wa Mungu katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. • Kutoa muhtasari wa utawala wa Mungu katika Maandiko, ukianza na Bwana kama muumba na mtegemezaji wa yote, na siri ya kuasi (uasi wa kishetani katika anga za mbinguni), ambao ulisababisha majaribu na anguko la wanadamu, na laana, lakini uliishia na ahadi ya Mungu ya kuponda kichwa cha nyoka kupitia Uzao wa mwanamke. Kama matokeo ya Anguko, ulimwengu uko vitani na Mungu ndiye Shujaa wa Vita. • Kuainisha mambo makuu yanayohusu Mungu kama Shujaa wa Kiungu katika Agano la Kale, ikiwa ni pamoja na Mungu kama shujaa anayeshinda uovu unaofananishwa na mto na bahari, Mungu akimshinda Farao na majeshi yake, Yeye aliyewaongoza watu wake katika ushindi kama Bwana mkuu wa majeshi, na ambaye alipigana dhidi ya watu wake mwenyewe kwa sababu ya ukaidi na uasi wao. Pia, manabii wa Israeli walimzungumzia Mungu kama shujaa wa kimungu ambaye hatimaye kupitia Masihi wake angeharibu uovu wote mara moja, milele. • Kuonyesha namna ambavyo ahadi ya Masihi kupitia “mrithi wa Daudi” iliwakilisha kusudi la Mungu la kuandaa mfalme ambaye angerudisha

2

Made with FlippingBook Annual report maker