https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 6 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
utawala kwa watu wake, atatawala mataifa kwa haki na uadilifu, na kuleta ujuzi wa Mungu duniani kote akiwa Bwana na Mfalme. • Kufafanua kupitia Maandiko kwamba utawala wa Mungu ulioahidiwa umezinduliwa kupitia nafsi na kazi ya Yesu Kristo, ambaye ndiye mtu wa ukoo wa Daudi ambaye atarejesha utawala wa Mungu. Ndani yake na mambo mbalimbali yanayohusiana na kuzaliwa kwake, mafundisho yake, miujiza yake, kufukuza pepo, matendo yake, kifo na ufufuo wake, Ufalme wa Mungu sasa uko hapa, tayari upo katika maisha ya Kanisa. • Kuelezea taswira ya “tayari/bado” ya Ufalme wa Mungu; ijapokuwa Ufalme wa Mungu umekuja kupitia utimilifu wa ahadi ya Kimasihi katika nafsi ya Yesu, Ufalme huo utakamilika tu katika Kuja kwake Mara ya Pili, wakati udhihirisho kamili na wa mwisho utakapotokea. Kanisa ni ishara na kionjo cha Ufalme uliopo leo, nalo limeidhinishwa kutangaza na kuonyesha ushindi wa Kristo juu ya Shetani na laana kama wakala na naibu wa Kristo. • Kuonyesha vipengele vikuu vya taswira ya Utume kama Vita vya Milki , vikijumuisha kuthibitishwa tena kwa utawala wa Mungu leo juu ya ulimwengu wake katika Yesu Kristo, Mungu kama Shujaa ambaye kupitia mpakwa mafuta wake ameshinda nguvu za ibilisi na athari za laana, na jinsi umisheni kupitia tawira hii unakuwa udhihirisho na tangazo la utawala wa Mungu hapa na sasa. Kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi ni kuendeleza utawala wa Mungu kwa kushuhudia kwamba Ufalme umekuja kupitia Yesu wa Nazareti. Efe. 5:25-32 – Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Mojawapo ya maajabu makuu ya Maandiko ni siri zake za kina ambazo zimefichwa katika maisha na uzoefu wa wahusika wake wakuu. Kwa maana halisi sifa hii ya Mapenzi ya Kiungu
2
Ibada
Made with FlippingBook Annual report maker