https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
7 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maandiko inaakisi uvuvio wake; tunaweza kupata mafundisho makuu kuhusu asili ya Mungu na uhusiano wake na watu wake kutokana na mambo tunayojifunza kupitia maisha na matendo ya wahusika wakuu wa Biblia. Mfano wa Adamu na Hawa, na muungano wao pamoja kama mume na mke ni kielelezo cha muungano mkuu kati ya Kristo na watu wake, ambao, kwa namna ya kushangaza kulingana na andiko hili, ni bibi-arusi wake. Ni somo la kustaajabisha sana kwetu leo, ambalo linafunua nia ya Mungu kwa wanadamu kama ilivyotimizwa katika Kanisa. Mungu Mweza wa Yote ameamua tangu mwanzo wa nyakati kukusanya kutoka miongoni mwa mataifa yote watu wawe milki ya pekee kwa njia ya Yesu wa Nazareti. Hapa andiko hili linafunua siri kuu: katika kiini cha ulimwengu kuna tamthilia ya ajabu ya ulimwengu, mapenzi ya kiungu , hadithi na hekaya ya kweli ya ajabu na ya kusisimua ya uhusiano wa upendo usiokoma kati ya Mungu Mwenyezi, na watu. Sisi ni mashahidi hai wa hilo, na kama watu tunaoamini katika kweli ya Injili kuhusu Yesu wa Nazareti, sisi pia tumekuwa sehemu ya watu hao, walioitwa na kuchaguliwa kuishi katika tamthilia hiyo ya mapenzi ya kiungu. Asili ya mapenzi haya ya kiungu ni nini? Unaiona katika Agano la Kale kati ya Mungu na watu wake Israeli: Isa. 62:5 – Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. Tena, tunasoma kuhusu azimio la Bwana la kupendezwa na watu wake kama bwana-arusi: Isa. 62:4 – Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. Wenye haki wa Bwana watapambwa kama bibi-arusi katika arusi – arusi yake. (Taz. Isaya 61:10 – Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu). Taswira hii ya ajabu inaonekana wazi zaidi katika tamthilia ya Kristo na Kanisa lake, Bwana wetu akiwa bwana-arusi na Kanisa kama bibi-arusi wake. Maandiko yafuatayo yanatoa sampuli ya rejea za Yesu kama bwana-arusi wa watu wake:
2
Made with FlippingBook Annual report maker