https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 7 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Mathayo 9:15 – Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. Yohana 3:29 – Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Ufunuo 21:2 – Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Uhusiano ulio wazi na wa moja kwa moja zaidi unaonekana katika andiko letu la msingi la kipengele hiki cha ibada: Waefeso 5:25-27 – Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Kulingana na andiko hili, upendo ambao mwanamume anao kwa mke wake unapaswa kujegwa kwa kufuata kielelezo cha upendo ambao Yesu anao kwa watu wake. Zaidi ya hayo, kiini na lengo la huduma zote za kitume linapaswa kuwa kuwaandaa watu wa Mungu kwa ajili ya sherehe na muungano unaokuja: “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2Kor. 11:2). Kristo analijenga Kanisa lake, kundi lake takatifu la wanafunzi kutoka duniani kote, vizazi vyote na nyakati zote, wale ambao yeye binafsi aliwanunua kwa ajili yake mwenyewe, na ambao watamtumikia, na milango ya kuzimu haitakuwa na uwezo wa kushinda mashambulizi yao (Mt. 16:15-19). Yeyote kati yetu ambaye ameenda harusini anajua tofauti ya muonekano wa kawaida wa bibi arusi na mwonekano wake akiwa amepambwa kwa ajili ya siku ya harusi! Vivyo hivyo, Mungu anamtayarishia Mwana wake bibi-arusi, watu, kusanyiko la kimungu ambalo litakuwa kando yake milele na kutawala pamoja naye katika Ufalme ujao. Hii inafanya iwe kawaida na rahisi kulielewa jukumu la umisheni: kazi ya umisheni ni kukusanya kwa ajili ya Kristo nafsi zilizosalia, ili kukamilisha idadi ambayo amepewa na Baba yake (Yn. 6:44). Kwa ufupi, hakuwezi kuwa na wokovu nje ya watu wa Mungu katika mwili wa Kristo. Ikiwa hakuna Kanisa, hapawezi kuwa na Ukristo, hakuna wokovu, hakuna tumaini kwa ulimwengu huu. Toleo la kimjini la msemo wa baba mkuu wa Kilatini, Cyprian, huweka hili wazi zaidi: “ Kama Kanisa si mama yako, basi Mungu si baba yako !” Ndiyo, na amina!

2

Made with FlippingBook Annual report maker