https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
7 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kama waamini, sisi ni sehemu ya siri hii kuu: taraja la kushiriki umilele na Ufalme pamoja na bwana-arusi wetu, ambaye pia ni Mwokozi na Bwana wetu, Bwana Yesu Kristo. Njia tunazotumia kukiri na kuishi katika uhusiano wetu na yeye si kwa kujitenga mbali na Kanisa, bali, kama sehemu yake, kama mshirika wa Kanisa la Mungu katika Yesu. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu hawaji kamwe kanisani isipokuwa kwa ajili ya ubatizo wao, ndoa zao, na mazishi yao, au, kama wengine wasemavyo, wanapototolewa, wanapounganishwa, na wanapoagwa! Katika mawazo yangu, hakuna Mkristo mwenye ufahamu na aliyejengwa kwenye msingi wa Biblia anayeweza kudai kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na kulikana ama kulipuuza Kanisa; mtu wa namna hiyo amechanganyikiwa kabisa, na pengine si Mkristo hata kidogo. Kuwa Mkristo ni kuwa mshirika kama bibi-arusi wa Kristo, na kuwa sehemu ya mapenzi ya kiungu. Kwa maana halisi, neno la “wawili kuwa mmoja” litakuwa halisi wakati wa utimilifu wa mambo yote katika Ujio wa Pili wa Kristo, lakini Kanisa linauishi muungano na ukaribu huu sasa, leo. Hakika, Kanisa limeunganishwa na kufungamanishwa kabisa ndani na katika nafsi ya Yesu wa Nazareti: tunafurahia utambulisho na ushirika kamili na Kristo. “Tunafanyika mwili mmoja katika Kristo” (1Kor. 6:15-17), tulibatizwa katika yeye (1Kor. 12:13), na tukafa pamoja naye katika kifo chake msalabani (Rum. 6:3-4). Zaidi ya hayo, tulizikwa pamoja naye kwa ubatizo katika mauti yake (Rum. 6:3-4), na tukafufuliwa pamoja naye katika ufufuo (Efe. 2:4-7). Tulipaa pamoja naye (Efe. 2:6), tumeketishwa pamoja naye katika ulimwengu wa roho (Efe. 2:6), na tunateseka pamoja naye katika maisha haya tunapomtumikia (Rum. 8:17-18). Hivi karibuni, tutatukuzwa pamoja naye (Rum. 8:17), tutafufuliwa ndani yake (1Kor. 15:48-49), na tutabadilishwa tufanane naye tutakapomwona wakati wa kutokea kwake (1 Yoh. 3:2). Kisha, tutarithi vitu vyote pamoja naye kama warithi pamoja naye (Rum. 8:17), na tutatawala milele pamoja naye kama watawala pamoja naye katika uliwengu mpya (Ufu. 3:21). Ni siri ya ajabu kama nini, kwa kweli, kwa wale “wawili kuwa mwili mmoja.” Chukua nafasi yako kama mwamini katika Kristo katika kundi la wanadamu wenye kuheshimiwa wanaounda Kanisa moja, takatifu, la kimitume, bibi-arusi wa Kristo, kundi hilo takatifu litakalotawala pamoja na Kristo katika Ufalme wake. Ni baraka iliyoje kuwa sehemu ya mapenzi ya kiungu. Karamu inakaribia kuwa tayari. Ufunuo 19:6-8 – Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. 7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
2
Je, umejiweka tayari? Utakuwepo?
Made with FlippingBook Annual report maker