https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 7 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu, Baba Mwenyezi uliyemchagua mtumishi wako Ibrahimu na kumfanya kuwa mwaminifu kutii wito wako na kufurahia ahadi yako kwamba jamaa zote za dunia zitabarikiwa ndani yake: Utujalie imani thabiti ili ahadi zako zitimie ndani yetu; kwa Yesu Kristo Bwana wetu. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni. Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 15.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo yako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 1, Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Kwanza.
Jaribio
2
Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Waebrania 6:17-18.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Kufufuka kwa Taswira ya Bibi-arusi
Katika baadhi ya makusanyiko ya kanisa la kiinjili leo, kuna kufufuka kwa taswira ya bibi-arusi katika maisha na ibada ya kanisa. Hata hivyo, kufufuka huko hakulengi kutumia taswira hiyo kuzungumzia kusanyiko la ushirika wa Mwili wa Kristo, bali taswira ya bibi-harusi inatumika kuzungumzia maisha ya mtu binafsi katika kutembea kwake na Kristo. Ili kupata hisia ya ukaribu na muunganiko wa kibinafsi unaotolewa na taswira hii, baadhi ya makusanyiko yanazingatia kwa karibu mada hii kama jambo la kibinafsi. Kwa mfano, walimu wanafundisha taswira ya bibi harusi kwa watu binafsi kuhusu safari yao binafsi na Mungu. Nyimbo za kuabudu na sifa zinaandikwa kwa kuzingatia ndoa ya kibinafsi ya mwamini na Kristo, na maisha ya kiroho yanatafsiriwa upya ili kuakisi kweli na mifano hii muhimu katika lugha za faragha binafsi. Kilicho wazi ni kwamba, hii imesababisha mkanganyiko
1
Made with FlippingBook Annual report maker