https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
7 4 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
fulani kuhusu ndoa ya Kristo, na ni kwa kiasi gani (kama ni lazima) taswira hii inaweza kuhusianishwa na watu binafsi. Je, una maoni gani kuhusu matumizi binafsi ya taswira hii kwa habari ya maisha binafsi ya mwamini? Je! matumizi kama haya yanatumia vibaya taswira hii, ambayo inapaswa kutumika kumaanisha zaidi “watu wa Mungu” na sio kwetu sisi kama tulioolewa kibinafsi na Kristo?
Siri ya Kuasi (Fumbo la Uovu)
Kwa sababu ya mafundisho ya kila aina katika duru fulani za Kikristo yanayotilia mkazo juu ya ufahamu wa masuala ya mapepo na ulimwengu wa giza, kumekuwa na maswali mengi kuhusu namna ambayo tunapaswa kuzungumzia na kufikiria juu ya nguvu za giza zinazotajwa katika Maandiko. Mitume walikuwa waangalifu kutokuingia kwa undani sana kuhusu utendaji wa ndani wa pepo, au kutoa pepo, au kutoa maelekezo juu ya mambo hayo; baadhi ya huduma leo, hata hivyo, zinaonekana kubobea katika mtazamo huu. Wakitafuta kuelewa baadhi ya haya mapepo yaliyoenea sana kila mahali na mikakati ya kushinda nguvu za giza, Wakristo wengi hujikuta wakilemewa katika maisha yao binafsi kwa kujishughulisha kwa ukaribu zaidi na mapepo, na ushawishi wake katika maisha yao. Wengine, kwa sababu ya kuogopa aina hii ya msisitizo kupita kiasi, wanapuuza kabisa ukweli kwamba Biblia inataja mara kwa mara na kuripoti kwamba Kristo mwenyewe na mitume wake walikabiliana na mapepo. Kwa kuzingatia vita tulivyo navyo dhidi ya watawala na wakuu wa giza, ni nini kinapaswa kuwa mtazamo wetu juu ya nguvu za giza ambazo Paulo anasema tunashindana nazo katika maisha yetu ya Kikristo? (rej. Efe. 6:11 na kuendelea). Je, tunapaswa kuchukuliaje maelezo kuhusu Shetani, roho waovu, na uovu kwa ujumla, na ni hatua gani au mwitikio gani unafaa kwetu kama Wakristo kuwa nao kuhusiana na mambo hayo? Kwa mujibu wa Paulo, kiini cha huduma ya kitume ni kuwatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya ndoa ijayo ya Kristo (2Kor. 11:2). Watu wa Mungu kwa kweli ni bibi-arusi wa Kristo, wanaotayarishwa naye ili wawe bibi-arusi mzuri na asiye na dosari, watu wasio na mawaa wala kunyanzi (Efe. 5), waliovikwa tayari kwa ajili ya siku ile kuu ya kuunganishwa wakati watu wa Mungu watakapokutana naye na kukaa naye milele (1 Thes. 4:13-17). Kwa maana halisi, utume na huduma zote zina ladha ya kipekee ya kieskatolojia: uinjilisti wote unafanya kazi ya kuongeza idadi ya bibi-arusi wa Mwana-Kondoo ambaye ataishi katika Yerusalemu Mpya; na kazi ya kufanya wanafunzi yote ni kuwatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya muungano huo mkuu na ndoa ya Mwana-Kondoo (Ufu. 19). Jaribu kupata picha Kiini cha Huduma ya Kitume
2
2
3
Made with FlippingBook Annual report maker