https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 7 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
ikiwa tutaichukulia huduma katika mtazamo huu wa kuhisi shauku na wivu wa kimungu kwa ajili ya wale tunaowatumikia na kuwahudumia, na kwamba tumepewa kazi ya kuwa washenga kwa niaba ya Mungu kwa ajili ya “kuwachumbia” watu wa Mungu kwa mume mmoja, ili kuwaleta kama bikira safi kwa Kristo (2 Kor. 11:2). Je, unadhani mtazamo huu unaweza au unapaswa kuathiri vipi uelewa wetu wa huduma? Je, inaweza kuathiri vipi mtazamo na utendaji wetu ikiwa tutaona umisheni na huduma kama jitihada ya kuwatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya muungano ujao na Kristo? Je, unadhani picha hiyo haina uhalisia sana, au ni picha inayotia nguvu na kufafanua kwa kiasi kikubwa kiini cha kazi ya umisheni?
Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Pili Sehemu ya 1: Utume kama Mapenzi ya Enzi
YALIYOMO
2
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake ni mojawapo ya sababu kuu za utume katika Maandiko Matakatifu, yaani, azimio la Mungu la kuvuta watu kutoka ulimwenguni ili wawe milki yake mwenyewe, milki iliyotimizwa na kukamilishwa katika upendo wa Yesu kwa Kanisa lake. Wazo la bwana-arusi na bibi-arusi katika Agano la Kale linajulikana sana, linahusishwa kwa ukaribu na wazo la muungano wa kijamii, furaha, na shangwe katika Maandiko, pia linatumika kama taswira ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake (kama inavyoonekana katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora). Hatimaye, watu wa Mungu wangerejeshwa kwake, na Yeye angecheza na kushangilia juu ya watu wake kama bwana-arusi afanyavyo juu ya bibi-arusi wake. Vidokezo vya tumaini na ahadi ya agano jipya vimejumuishwa katika agano la Mungu na Ibrahamu, na matarajio yake ya kujumuishwa kwa Wasio Wayahudi. Katika Yesu Kristo, taswira ya bwana-arusi imepanuliwa na kukamilishwa. Yesu sasa amekuwa chanzo na uzima wa Kanisa, bibi-arusi wake mpya, na Yohana Mbatizaji, mtangulizi wake, amekuwa rafiki wa bwana-arusi. Siri ya mwili sasa imefunuliwa kupitia mitume na manabii, kwamba Mataifa ni warithi pamoja na Wayahudi katika ahadi ya agano jipya la Mungu, na kupitia hilo, wanakaribishwa kama washiriki wa jamii mpya ya watu wa Mungu na bibi arusi wa Kristo. Mapenzi ya kiungu yatakamilika kwa kushuka kwa Yerusalemu Mpya kutoka mbinguni, makao ya Mungu na watu wake, ambao watajitambulisha kikamilifu na Kristo, bwana-arusi, kwa kubadilishwa na kufanana naye, kuwa warithi pamoja naye, na kukaa katika uwepo wake milele kama watawala pamoja naye. Kwa hiyo, utume ni kazi ya kueneza ujumbe huu wa Mungu kuchagua watu
Muhtasari wa Sehemu ya 1
Made with FlippingBook Annual report maker