https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

7 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kutoka katika mataifa yote, ambao kwa imani katika Yesu Kristo wanafanyika washiriki wa jamii ya ufalme wake, ambao wataishi pamoja naye milele. Lengo letu katika sehemu hii, Utume kama Mapenzi ya Enzi , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake ni mojawapo ya sababu kuu za utume katika Maandiko Matakatifu, yaani, azimio la Mungu la kuvuta watu kutoka ulimwenguni ili wawe milki yake mwenyewe, milki iliyotimizwa na kukamilishwa katika upendo wa Yesu kwa Kanisa lake. • Dhana ya bwana-arusi na bib-arusi ni maarufu katika Agano la Kale, inahusiana na wazo la muungano wa kijamii, furaha, na shangwe katika Maandiko, pia inatumika kama taswira ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake (kama inavyoonekana katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora). • Dhana ya Israeli kama bibi-arusi wa Mungu inaanza na uhusiano wa Mungu na Israeli katika asili yake duni na ya kupuuzwa, kwa uteuzi wa neema wa Mungu, uchumba na ndoa, uzinifu wa Israeli, kutoamini na ibada za sanamu, na ukosefu wa haki, hadi hukumu ya Mungu na uhamisho na utumwa wa Israeli (Ufalme wa Kaskazini), na Yuda (Ufalme wa Kusini). • Kurudi kwa watu wa Mungu katika nchi kulianza kwa amri na ruhusa ya Mfalme Koreshi ya kuingia tena katika nchi, ambayo ilitekelezwa kupitia Ezra, Zerubabeli, na Nehemia. Mungu aliwaahidi watu wake kwamba angefanya nao agano jipya, ambalo halikuwa kwa msingi wa utii na uaminifu wao bali kwa kuandika sheria yake mioyoni mwao na kuwapa roho mpya. Hatimaye, watu wa Mungu wangerudishwa kwake, na siku moja angecheza na kushangilia juu ya watu wake kama bwana-arusi afanyavyo juu ya bibi-arusi wake. • Vidokezo vya tumaini na ahadi ya agano jipya vimejumuishwa katika agano la Mungu na Ibrahamu, na matarajio yake ya kujumuishwa kwa mataifa. Katika Yesu Kristo, taswira ya bwana-arusi imepanuliwa na kukamilishwa. Yesu sasa amekuwa chanzo na uzima wa Kanisa, bibi-arusi wake mpya, na Yohana Mbatizaji, mtangulizi wake, amekuwa rafiki wa bwana-arusi. • Muundo kamili wa watu wa Mungu ulifunuliwa kupitia kufunuliwa kwa siri kupitia mitume na manabii, kwamba Mataifa ni warithi pamoja na Wayahudi katika ahadi ya agano jipya la Mungu, na kupitia hilo, wanakaribishwa kama washiriki wa jamii mpya ya watu wa Mungu na bibi arusi wa Kristo.

2

Made with FlippingBook Annual report maker