https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 7 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

• Mataifa wote (kama Wayahudi) wanakaribishwa katika mwili (Kanisa) na bibi-arusi wa Kristo kwa imani, kuoshwa katika damu yake na kujumuishwa katika Kanisa la Mungu. Mataifa hawana haja ya kukana utambulisho wao wa kitamaduni kama ilivyofafanuliwa katika Baraza la Yerusalemu (rej. Mdo. 15), na sasa kiini cha huduma zote za kitume ni kuwatayarisha watu wa Mungu kama bibi-arusi, ambaye Kristo atampokea wakati wa kuja kwake, bila mawaa machoni pake. • Mapenzi ya kiungu yatakamilika kwa kushuka kwa Yerusalemu Mpya kutoka mbinguni, makao ya Mungu na watu wake, ambao watajitambulisha kikamilifu na Kristo, bwana-arusi kwa kubadilishwa na kufanana naye, kuwa warithi pamoja naye, wakiwa katika uwepo wake milele kama watawala pamoja naye. • Kwa habari ya utume, vipengele vikuu vya mapenzi ya kiungu ni hivi: Mungu anavuta watu kutoka katika mataifa yote kwa ajili yake, ambao ni pamoja na Wayahudi na mataifa. Kwa hiyo, utume ni kazi ya kueneza ujumbe huu wa Mungu kuchagua watu kutoka katika mataifa yote ambao, kwa imani katika Yesu Kristo, wanafanyika washiriki wa jamii ya ufalme wake ambao wataishi pamoja naye milele.

2

I. Utume kama Mapenzi ya Enzi: Azimio na shauku ya Mungu ya kutoa watu kutoka miongoni mwa mataifa ili wawe wake na kumtumikia Yeye milele.

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

Muungano wa Kiagano kati ya Mungu na Watu wake

Agano Jipya linachukua mada ya Agano la Kale inayohusu agano kati ya Mungu na wanadamu kama mfumo ambamo uhusiano wa Mkristo na Mungu na uhusiano wa kanisa na Mungu kupitia Kristo unaeleweka. Wakristo wameunganishwa naye katika uhusiano wa agano uliojengwa juu ya ahadi bora na msingi thabiti kupitia kazi ya Kristo kwa niaba yetu. Picha ya ndoa, iliyotumiwa na baadhi ya manabii wa Agano la Kale kuelezea agano la Mungu na watu wake, inachukuliwa katika Agano Jipya na kutumika kwa Kristo (Bwana-arusi) na kanisa (bibi-arusi wake). Hii inasisitiza asili ya muungano wa agano kama upendo wa pande zote wa kujitoa kwa dhati, kuheshimiana, uaminifu na utii wa kweli. (Picha zingine za uhusiano wa

Made with FlippingBook Annual report maker