https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

7 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kifamilia pia zinatumika, kama baba/mwana, na kaka mkubwa na watoto wengine). Wapuritani, miongoni mwa wengine, walipendelea mada hii hasa. ~ J. P. Baker. “Union With Christ.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 698.

A. Dhana ya bibi-arusi na bwana-arusi katika matumizi ya Agano la Kale

1. Maneno “Bibi-arusi” na “bwana-arusi” yametumika pamoja kwa kuhusianishwa katika Yohana 3:29.

2

2. Maneno haya yanaonekana pamoja katika maandiko kadha wa kadha, daima yakiunganishwa na wazo la “sauti ya furaha na shangwe” inayohusishwa na wazo la furaha ya ndoa (rej. Isa. 62:5; Yer. 7:34; 16:9; 25:10; 33:11; Ufu. 18:23).

3. Picha ya msingi ya uhusiano wa Mungu na watu wake: Bwana ni mume wa watu wake, Isa. 54:5.

4. Bwana aliwachagua watu wake Israeli, si kwa sababu ya ukuu wao au utajiri wao, bali kwa sababu ya upendo wake mwingi kwao, shauku yake kwao kuwa watu wake maalum, Kum. 7:6-10.

a. Kut. 19:5-6

b. Kumb. 14:2

c. Kumb. 26:19

d. Kumb. 28:9

Made with FlippingBook Annual report maker