https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 8 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

3. Katika bibi-arusi wa Kristo, kuwa Myahudi au Mmataifa haimaanishi chochote kwa kuwa Kristo ni yote (Kol. 3:11).

Hitimisho

» Tangazo la ufalme kwa Mataifa linapanua nia ya Mungu ya kuvuta watu kutoka duniani kote kuwa milki yake mwenyewe. » Kwa imani katika Yesu Kristo, sasa hata watu wa mataifa wanaweza kushiriki katika mpango wa ajabu wa Mungu wa kujikusanyia watu ambao wataishi pamoja naye milele. » Utume unashiriki katika mapenzi haya ya kiungu, kuandaa watu ambao watakuwa wa Mungu milele. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yamejitokeza kupitia video. Katika sehemu hii tumeona namna ambavyo katika taswira ya Utume kama Mapenzi ya Enzi Mungu aliamua kuvuta wa kutoka duniani kote ambao watakuwa milki yake na kumtumikia milele. Kupitia siri iliyofunuliwa kupitia mitume na manabii, sasa tunaona jinsi ambavyo Mungu amepanua tangazo la ufalme kwa watu wa mataifa mengine, ambao wamefanyika warithi na viungo vya mwili wa Kristo na bibi-arusi wa Kristo. Kwa imani katika Yesu Kristo, sasa hata watu wa mataifa wanaweza kushiriki katika mpango wa ajabu wa Mungu wa kuumba watu ambao wataishi pamoja naye milele. Utume unashiriki katika mapenzi haya ya kiungu kwa kuandaa watu ambao watakuwa wa Mungu milele. Kuelewa vipengele vya taswira hii kunaweza kukusaidia sana kuelewa kile ambacho umisheni unatafuta kufanya kupitia juhudi zake mbalimbali. Kwa sababu hiyo tafadhali pitia maarifa ambayo tumejifunza hivi punde kwa kutumia maswali yaliyo hapa chini, na unukuu Maandiko ili kuunga mkono majibu yako. 1. Fafanua kwa ufupi taswira ya Utume kama Mapenzi ya Enzi . Taswira ya mapenzi ya kiungu kati ya Mungu na watu wake inadhihirishaje azimio la Mungu kwa ajili yake mwenyewe na ulimwengu wake? Eleza. 2. Fuatilia wazo la bibi-arusi na bwana-arusi katika Agano la Kale. Ni katika maana gani picha hii ni wazo kuu katika suala la uhusiano wa Mungu na watu wake? Wimbo Ulio Bora unahusianaje na mada hii?

2

Sehemu ya 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook Annual report maker