https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
8 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
III. Dondoo za mwisho za utume kama Mapenzi ya Enzi
A. Shauku ya Mungu ni kuvuta watu ambao watakuwa wake milele kutoka katika mataifa yote, yaani pamoja na wasio Wayahudi.
1. Hili lilikuwa ni utimilifu wa Maandiko kuhusu Masihi, Luka 24:45-47.
2. Tangazo hili la wokovu wa Wayahudi na Mataifa lilipaswa kuanza na Wayahudi, lakini litangazwe hata miisho ya dunia, Mdo 1:8; taz. Mdo 2:32-; 3:15-16; 4:33; Mdo 8:5-35; Rum. 10:18; 15:19.
2
B. Mungu anawapenda wanadamu wote, si watu wake Israeli pekee: haya ndio maono makuu ya mapenzi ya kiungu ya Mungu.
1. Zab. 22:27
2. Isa. 52:10
3. Rum. 10:18
C. Utume ni ushuhuda kwa mataifa yote kwamba Mungu wa Wayahudi ni Mungu wa Mataifa pia! Rum. 3:29-30.
1. Watu wa Mataifa watajumuishwa ndani ya bibi-arusi mtakatifu wa Mungu na kumtolea sifa, Rum. 15:9-13.
2. Kufunuliwa kwa Siri: Mataifa ni warithi wenza na washirika katika mwili mmoja: utume unawahubiria Habari Njema, Efe. 3:6.
Made with FlippingBook Annual report maker