https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 9 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
katika Yesu Kristo, na kupitia wakala wake, Kanisa. Mungu ndiye Shujaa ambaye kupitia mpakwa mafuta wake amezishinda nguvu za shetani na madhara ya laana. Utume ni udhihirisho na tangazo la utawala wa Mungu hapa na sasa, na kufanya mataifa kuwa wanafunzi ni kuendeleza utawala wa Mungu kwa kushuhudia kuja kwake katika nafsi ya Yesu wa Nazareti.
I. Utume kama Vita vya Milki: Mungu kama Shujaa anayesimamisha utawala wa Ufalme wake juu ya ulimwengu.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
Utume Unatangaza Vita vya Mungu dhidi ya Ibada ya Sanamu Swali la msingi la theolojia: ‘Tunamaanisha nini tunapotaja neno «Mungu,»’ linaweza kujibiwa katika mitazamo mbalimbali kwa kuchunguza namna mbalimbali ambazo Mungu amejihusisha na ulimwengu na sisi wenyewe. Jambo la kushangaza ni kwamba, kujifunza kuhusu ibada ya sanamu kunatupatia pia ufahamu fulani kuhusu asili ya Mungu wa kweli. Je! Sifa ya kuitwa “mungu” inatokana na nini? Jibu la Martin, Luther alipokuwa akitafakari juu ya amri ya kwanza katika katekisimu yake kubwa zaidi, lilikuwa : ‘chochote ambacho moyo wako unashikamana nacho na kukitegemea, huyo ndiye Mungu wako; tumaini na imani ya moyo peke yake ni msingi wa kigezo cha kuitwa au Mungu ama [mungu] sanamu’. Tunataka kuthibitisha maoni yake, lakini pia kusisitiza kigezo cha upendo na huduma: mungu ni yule unayempenda, unayemwamini na kumtumikia zaidi ya yote. Ufafanuzi huu unadokeza uwezekano na ulazima wa haraka wa kuweka wazi ukubwa wa tatizo la ibada ya sanamu katika ulimwengu wa sasa. Kwa maana moja ibada ya sanamu ni utambuzi wa ile hali ya kibinadamu ambayo Injili ni tiba yake. Shida kuu ya wanadamu sio shida ya «kijamii» kati ya mtu na mtu mwingine (kama uasherati au uchoyo), bali ni uasi dhidi ya Mungu na kutoa nafasi ya Mungu wa kweli na aliye hai kwa miungu inayoshindwa (jambo ambalo husababisha dhambi hizi za uharibifu). Ikiwa hadithi ya wanadamu ni hadithi ya kusikitisha ya aina tofauti tofauti za ibada ya sanamu, ambayo ni kilele cha upumbavu wa mwanadamu, Habari Njema ni kwamba Mungu huwapatanisha wabeba-sura yake na nafsi yake mwenyewe katika Kristo. Si kwa bahati kwamba manabii waliutarajia wakati ambapo sanamu zitakomeshwa na mahali pake patachukuliwa na ibada ya kweli. ~ Brian S. Rosner. “Idolatry.” The New Dictionary of Biblical Theology . T. D. Alexander, mh.(toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001.
2
Made with FlippingBook Annual report maker