Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kutoka kwenye kushughulika na mataifa kwa ujumla na kulielekea taifa teule hasa. Taifa hili lilianza na Abrahamu (sura ya 12-24), liliendelea kupitia mwanawe Isaka (sura ya 25-27), na kupitia mwana wa Isaka, Yakobo (sura ya 28-36). Watu hawa walihifadhiwa kimuujiza na Yusufu (sura ya 37-50), na, kupitia uangalizi na utunzaji wa Mungu, familia nzima

ya Yakobo ilishuka mpaka Misri. Kutoka: Ukombozi wa Taifa

Mapenzi makamilifu ya Mungu yalikuwa kwamba taifa lililochaguliwa libaki katika Nchi ya Ahadi na “kutoshuka kwenda Misri” (Mwa. 26:2). Hata hivyo, katika mapenzi maruhusiwa ya Mungu, Alimwambia Yakobo, “usiogope kushuka mpaka Misri” (Mwa. 46:3), ili katika mapenzi yake ya uandalizi na kwa tendo la ukombozi, Mungu aweze kusema, “alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri” (Hosea 11:1). Sehemu ya kwanza ya Kutoka ilirekodi ukombozi wa taifa (sura ya 1-18), na sehemu ya mwisho ilirekodi ufunuo wa taifa (sura ya 19-40) katika vibao vya Torati (sura ya 19-24), ukifundisha utii, na katika hema (sura ya 25-40) ukifundisha ibada. 7 Walawi: Utakaso wa Taifa “Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu” (19:2) ndilo wazo kuu katika kitabu chote. Katika Mwanzo, Israeli ilichaguliwa kwa ajili ya haki; katika Kutoka, walitangazwa kuwa wenye haki kwa njia ya ukombozi; na katika Mambo ya Walawi, Mungu alitaka kuwafanya wenye haki kwa njia ya utakaso. Katika Kutoka waliingizwa katika muungano na Mungu; katika Mambo ya Walawi waliongozwa ili wawe na ushirika naye. Kutoka inaonyesha msamaha wao, na Mambo ya Walawi usafi au utakatifu wao. Sehemu ya kwanza ya

7 Mengi ya maelezo (muhtasari) yaliyotumiwa hapa yamechukuliwa kutoka kwa W. C. Scroggie, Know Your Bible (New York: Revell, 1940).

102

Made with FlippingBook Digital Publishing Software