Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

TORATI: MSINGI KWA AJILI YA KRISTO Kufuatia mgawanyo wa sehemu nane wa Biblia yetu ya sasa, sehemu nne za Agano la Kale zinamtazamia Kristo kwa matarajio, na sehemu nne za Agano Jipya zinamwonyesha Kristo katika utimilifu. Kristo anaweza kuonekana katika Agano la Kale katika matarajio kwa njia nne za msingi: (1) Torati iliweka msingi wa kuja kwa Kristo; (2) Historia ilifanya matayarisho kwa ajili yake; (3) Mashairi yalitazama juu kwa matamanio ya ujio wake; (4) Manabii waliona mbele kwa matazamio ya ujio huo. Vitabu vya Torati viliweka msingi kwa ajili ya Kristo kwa kuwa viliandika matayarisho ya taifa la Kimasihi ambalo kupitia kwalo Kristo angekuja na ambaye angetawala akiwa Mfalme juu yake. Mpango wa Mungu ulikuwa wa kubariki “jamaa zote za dunia” (Mwa. 12:3), lakini alichagua taifa moja ambalo kupitia hilo angetimiza kusudi hilo. Kwa hiyo, katika maana ya jumla ya neno hili, Kristo ni mada ya Agano la Kale lote kwa njia isiyo ya moja kwa moja, katika maana ya maandalizi ya taifa ambalo lingemleta Masihi. Bila shaka, Kristo yuko katika Agano la Kale kwa njia nyingi zaidi kuliko njia ya maandalizi ya jumla. Yuko humo pia kwa njia ya unabii na mifano ya awali (vivuli, nk., rej. sura ya 2). Hapa, hata hivyo, mkazo hasa hasa uko kwenye maandalizi ya jumla kwa ajili ya Kristo katika Agano la Kale, kama inavyoonekana kupitia mgawanyo wa sehemu nne. Mwanzo: Kuchaguliwa kwa Taifa Hatua ya kwanza katika maandalizi ya Kristo ilikuwa ni kuchaguliwa kwa taifa ambalo lingekuwa njia ambayo Kristo angekuja. Sura ya 1-11 ya Mwanzo inatoa taswira fupi ya uumbaji (sura ya 1-2), na uharibifu wa mataifa (sura 3-6) na matokeo ya maafa ya gharika (sura ya 7-9). Kufuatia hili, laana ya Mungu iliangukia ustaarabu wa Wakanaani Babeli (sura ya 10-11). Katika sura za mwisho za Mwanzo (sura ya 12-50), Mungu aligeuka

101

Made with FlippingBook Digital Publishing Software