Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Vitabu hivi vitano vya Torati viliweka msingi wa ujio wa Kristo si kitaifa tu kwa namna vilivyofunua historia ya taifa ambalo lingemzaa Masihi, lakini pia kitheolojia , kwa kuwa Kristo ndiye Mwenye kuchagua (Mwanzo), Mkombozi (Kutoka), Mtakasaji (Mambo ya Walawi), Kiongozi (Hesabu), na Mwalimu (Kumbukumbu la Torati). HISTORIA: MAANDALIZI KWA AJILI YA KRISTO Katika Torati, Mungu alitenda juu ya taifa lake. Katika Historia taifa hilo linaanza kutenda kwa ajili ya Mungu. Musa alikuwa amewatoa Israeli kutoka utumwani lakini Yoshua akawaongoza katika baraka . Musa aliwapa sheria yao, Yoshua akawapa nchi yao. Msingi uliwekwa katika Torati, na hapa matayarisho yanafanywa kwa ajili ya Kristo katika historia ya Israeli. Yoshua: Umiliki wa Taifa Baada ya kifo cha Musa, Mungu alimwambia Yoshua, “ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli” (Yos. 1:2). Mara moja wakaingia katika nchi (1:1-5:12), wakateka nchi (5:13-12:24), wakamiliki nchi (sura ya 13-25). “Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote Bwana aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao” (11:23). Waamuzi: Ukandamizwaji wa Taifa Kitabu cha Waamuzi kilihamisha historia kutoka ushindi hadi uasi imani. Hapo mwanzo taifa hilo lilikuwa limeyashinda mataifa ya nchi, lakini baadaye lilipigwa na mataifa hayohayo. Israeli waligeuka kutoka kwenye uaminifu hadi kutokuwa na imani. Wakati taifa lilipokumbana na kushindwa kwa muda katika maandalizi yake kwa ajili ya Kristo, lilionyesha wakati huo huo hitaji la wazi zaidi la Mwokozi-Mtawala.
104
Made with FlippingBook Digital Publishing Software