Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Sababu ya waamuzi kuhitajika ni uasi wa Israeli (1:1-3:8). Utawala wa waamuzi ulikuwa wa uaminifu-mshikamanifu wa hapa na pale (3:9— 16:31), na uharibifu wa mwisho wa waamuzi ulikuja kwa machafuko ya kitaifa (sura ya 19-21), wakati “kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema machoni pake mwenyewe” (21:25). Kwa ujumla, taifa lilipitia mizunguko saba, kila mmoja ukijumuisha dhambi, utumwa, dua na wokovu (taz. 2:16-). Ruthu: Kisa cha Kujitoa ndani ya Taifa Utofauti wa kipekee na dhahiri kwa uchafu wa wakati wa waamuzi ni usafi wa Ruthu. Kitabu hiki kinaonekana kama yungiyungi kwenye bwawa la matope la waamuzi. Ni hadithi ya kujitoa katika siku ya kushuka na kudhoofu, hadithi ya uaminifu katikati ya kipindi cha utovu wa uaminifu. Ruthu akawa bibi wa Daudi (4:22) ambaye kupitia kwake Masihi angekuja. 1 Samweli: Uimarishwaji wa Taifa Hali ya kukosa utulivu na machafuko ya waamuzi vilitoa nafasi kwa uthabiti wa ufalme wa Sauli. Uamuzi wa Samweli (sura ya 1-7) ndio ulitengeneza daraja kati ya waamuzi na ufalme wa Sauli (sura ya 8-15). Lakini watu, wakiwa na nia mbaya, walikuwa wamelalamika wakihitaji mfalme (1 Sam. 8:5), na chaguo lao la mfalme lilitokana na kabila lisilofaa (Benyamini badala ya Yuda). Matokeo yake, Sauli, chaguo la watu, ilimbidi kumwachia Daudi , chaguo la Mungu (sura 16-31). Kwa ujio wa Daudi walipokea mfalme ambaye Mungu alimtaka (1 Sam. 13:14). 2 Samweli: Upanuzi wa Taifa Wakati wa utawala wa Daudi (2 Samweli) na Sulemani (1 Wafalme 1-10), mipaka ya Israeli ilipanuliwa na hekalu lake kujengwa. Umaarufu wa Daudi ulionyeshwa kwa kutambuliwa kwake kwenye kiti cha enzi (sura 1-10). Hata hivyo, aibu yake ilisababisha kukataliwa kwake na kiti cha enzi

105

Made with FlippingBook Digital Publishing Software