Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
(sura 11-18), lakini hatimaye jina la Daudi lilihifadhiwa kwa kurejeshwa kwake kwenye kiti cha enzi (sura 19-24). Msingi ulikuwa umewekwa kwa ajili ya Kristo katika Torati, lakini hapa katika Historia maandalizi yalifanywa kwa ajili ya Kristo, ambaye angekuja kama Mwana wa Daudi na kutawala katika Yerusalemu (2 Sam. 7:12-). 1 Wafalme: Kuzorota kwa Taifa Katika mstari wa kwanza wa 1 Wafalme 11 maneno haya ya kutisha yanatokea, “ Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni.” Tokea wakati huo kuzorota kwa ufalme kulionekana wazi. Ufalme ulioungana wa Sulemani (sura ya 1-11) ulizaa falme zilizogawanyika za Israeli na Yuda (sura ya 12-22). Wakati wa kifo cha Sulemani jemadari wake, Yeroboamu, aliasi pamoja na makabila kumi ya kaskazini yaliyoitwa Israeli, huku mwanawe Rehoboamu akiwa mfalme juu ya makabila ya kusini ya Yuda na Benyamini ambayo yaliitwa Yuda. 2 Wafalme: Kufukuzwa kwa Taifa Kulikuwa na sababu tatu za msingi zilizo sababisha Israeli kuangukia katika mikono ya Waashuru mwaka wa 722 B.K. na Yuda wakaangukia kwa Wababiloni mwaka wa 586 B.K. • Kidini, kulikuwa na ibada ya sanamu (rej. 1 Wafalme 11:4; 12:28-29). • Kimaadili, uasherati ulikuwa jambo la kawaida (1 Wafalme 11:1-11; 14:24). • Kisiasa, mfarakano ulikuwa umeligawanya taifa katika sehemu mbili (1 Wafalme 12:16-19). Rekodi ya kushuka na kuchukuliwa utumwani kwa Israeli (sura 1-17) haina hata mfalme mmoja mzuri. Katika kudhoofika na kuchukuliwa kwa Yuda (sura 18-25) kuna tofauti chache tu zinazojulikana kuhusu picha hii mbaya ya enzi ya kifalme isiyo na haki. Lakini tofauti hizi hazingeweza
106
Made with FlippingBook Digital Publishing Software