Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

kupingana na wimbi kubwa la uovu, na hata Yuda walichukuliwa utumwani kwa miaka sabini (2 Wafalme 24:2), kama vile nabii Yeremia alivyotabiri (25:11). I na II Mambo ya Nyakati: Historia ya Taifa Inarudiwa Wafalme kimsingi ni historia ya kisiasa, wakati Mambo ya Nyakati ni historia ya kidini. Wafalme imeandikwa kwa mtazamo wa kinabii, na Mambo ya Nyakati kutoka kwa makuhani. Mambo ya Nyakati ya Kwanza inalingana na 1 na 2 Samweli, na 2 Mambo ya Nyakati inalingana na 1 na 2 Wafalme, ingawa Mambo ya Nyakati inahusika na Yuda pekee. Esther: Uhifadhi wa Taifa Ingeonekana kana kwamba kusudi la Mungu la Kimasihi kwa taifa lilipotezwa na kushindwa na kutekwa kwa Yuda na Wababiloni, lakini haikuwa hivyo. Taifa lilitekwa lakini halikuharibiwa. Licha ya hatari kubwa sana mikononi mwa Hamani Mwajemi (sura ya 1-4), walipata ukombozi mkubwa kupitia Esta (sura ya 5-10). Na ijapokuwa jina la Mungu halimo katika kitabu hiki, mkono wa Mungu unadhihirika katika kuwahifadhi watu wake. Maandalizi kwa ajili ya Masihi yaliendelea kwa njia ya kuhifadhiwa kwa taifa la Kimasihi (rej. 4:14). Ezra: Urejesho wa Taifa Licha ya ukweli kwamba taifa lilikuwa limedhoofika na kutekwa, hata hivyo lililindwa na Mungu ili watu warudishwe na kurejeshwa katika nchi yao. Mungu aliuchochea moyo wa mfalme Koreshi mwaka wa 539 K.K. na karibu Wayahudi 50,000 walirudi chini ya Zerubabeli (sura ya 1-6). Baadaye, mwaka wa 458 K.K., takriban watu 2,000 zaidi walirudi chini ya Ezra (sura ya 7-10), watu waliporudishwa makwao.

107

Made with FlippingBook Digital Publishing Software