Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Nehemia: Kujenga Upya Taifa Katika Ezra, Yuda ilijenga upya maisha yake ya kidini (hekalu), lakini katika Nehemia maisha yake ya kisiasa yalijengwa upya. Kujengwa upya huku hakukuhusisha tu kujenga upya mji (sura 1-7), bali pia uamsho wa wananchi (sura 8-13). Kila kitu kilirejeshwa isipokuwa mfalme. Zaidi ya miaka mia nne ya “kimya” ilipita kabla ya “utimilifu wa wakati” (Gal. 4:4) wa Kristo kutokea na watu kuuliza, “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi?” (Mt 2:2). USHAIRI: MATAMANIO YA UJIO WA KRISTO Torati ina mtazamo wa kushuka chini kwenye msingi wa Kristo, Historia ina mtazamo wa nje katika maandalizi ya Kristo, lakini Ushairi una mtazamo wa juu katika matamanio ya ujio wa Kristo. Ingawa Torati inahusu maisha ya kiadili ya Israeli, na Historia inafunua maisha yao ya kitaifa, vitabu vya mashairi vinahusu maisha yao ya kiroho au ya kivitendo. Ayubu: Matarajio ya Upatanishi wa Kristo Ayubu alitamani mtu ambaye “angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu” (16:21). Tamaa yake ilikuwa mtu mmoja awe mpatanishi ambaye angeweza “kutuwekea mkono sote wawili,” yaani Mungu na mwanadamu (9:33). Aliuliza ikiwa kulikuwa na maana yoyote ya kuteseka, kusudi lolote la maumivu, au maana yoyote kwa taabu ya kibinadamu. Jambo ambalo Ayubu hakulitambua katika kina cha kukata tamaa kwake ni kwamba chochote kitakachotokea kwenye “eneo la tukio” (sura 3-41) kinaweza tu kueleweka kikamilifu katika mwanga wa kile kinachotokea “nyuma ya pazia” (sura 1-2), ambapo mshitaki wa ndugu anawashitaki mchana na usiku mbele ya Mungu, na kwa kuzingatia yale yatakayokuwa malipo yao “baada ya tukio” (sura 42). Zaidi ya hayo, kile ambacho Ayubu alitamani, bila kukielewa kikamilifu, kilikuwa ni Wakili (1 Yh. 2:1) au Kuhani Mkuu

108

Made with FlippingBook Digital Publishing Software