Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

ambaye angeweza “kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu” (Ebr. 4:15). Hakutambua kwamba umuhimu wa mateso ungepatikana katika dhabihu mbadala ya Mwokozi ambaye “aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1 Pet. 3:18). Kwa ufupi, kile ambacho Ayubu alitamani sana kilikuwa ni “mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu …mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” (1 Tim. 2:5). Zaburi: Matamanio ya Ushirika na Kristo Ingawa Ayubu anajadili “sababu” ya msiba, Zaburi zinasisitiza “namna” ya uchaji wa Mungu. Maombi na sifa, lugha ya kimungu ya nafsi, vimejaza kurasa za Zaburi. Ushirika huu na Mungu hauhusiani tu na uumbaji wake (Zab. 1-41), bali na ukombozi wake (Zab. 42-72), na patakatifu pake (Zab. 73-89), na utunzaji wake (Zab. 90-106), pia na maadili yake (Zab. 107-50). Wakati fulani shauku hii ya ushirika na Kristo katika Zaburi inachipuka na kuwa matamko ya wazi ya Kimasihi kuhusu Kristo (taz. Zab. 22). Hata hivyo, matamanio ya zaburi hayatimizwi hadi njia inapofunguliwa na Kristo mwenyewe kupitia kujishusha, kusulubishwa, ufufuo na maombezi yake, ili watu waweze kukaribia “kiti cha neema kwa ujasiri” (Ebr. 4:16). Mithali: Matamanio ya Hekima katika Kristo Hekima hii ilikuwa “busara katika utendaji” au aina ya “akili takatifu” ambayo iliwawezesha waamini sio tu kuifahamu kweli katika akili zao bali kuitumia kweli katika maisha yao. Matamanio katika Mithali ni hekima kufanyika mwili (Mith. 8), na ndivyo kweli ilivyokuwa wakati “hazina zote za hekima na maarifa” zilipofanyika mwili katika Kristo (Kol. 2:3). Kwa hiyo katika Mithali matamanio ni ya kupata hekima kama inavyoonyeshwa katika maneno kuwaelekea wenye hekima (sura ya 1-9), ya wenye hekima (10:1-22:16), kwa ajili ya wenye hekima (22:17-24:34), kutoka kwa wenye hekima (sura 25-31). Lakini kile ambacho watakatifu wa

109

Made with FlippingBook Digital Publishing Software