Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Agano la Kale walitamani kuwa nacho katika kanuni, watakatifu wa Agano Jipya walikuwa nacho katika mwili, kwa sababu ya Kristo Mwenyewe
“aliyefanywa [kwao] kuwa hekima…” (1 Kor. 1:30). Mhubiri: Matamanio ya Kuridhika katika Kristo
Wanafalsafa daima wamekisia juu ya asili ya “kilicho bora zaidi” ( summum bonum ). Wakati mwalimu mwenye hekima wa Mhubiri alipoanza kuitafuta, aliitafuta kwanza kwa uzoefu (sura 1-2), kwa kujaribu mvinyo, wanawake na kazi. Hata hivyo, aligundua kwamba hayo yote yalikuwa ni ubatili tu na kujilisha upepo. Kisha akachungunza suala hilo kifalsafa (sura 3-12), kwa njia ya mali na hekima, na kufikia hitimisho linalofanana na la kwanza: hakuna furaha “chini ya jua.” Alijifunza kwamba furaha lazima ipatikane nje ya jua, ndani ya Mwana, kama aandikavyo, “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu” (12:13), akisema kwamba maneno haya “yatoka kwa mchungaji mmoja” (12:11). Kwa hiyo, shauku yake ni kwa ajili ya Mchungaji Mwema (Yh 10), na kwa manufaa makubwa zaidi, ambayo katika Agano Jipya yanapatikana katika “mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (Flp. 3:14). Wimbo Ulio Bora: Matamanio ya Muungano na Kristo Kiuhalisia, wimbo huu unazungumza juu ya muungano wa kina wa ndoa. Hata hivyo, kiroho Wimbo Ulio Bora ni picha ya uhusiano kati ya Israeli na Yehova, au kati ya Mungu na mtu binafsi. Kuna ukomavu unaokua katika muungano wa upendo unaoendelea kutoka hatua ya kuwa na Mpendwa (2:16) hadi kumilikiwa na Mpendwa (6:3), hadi kufikia utambuzi kamili wa shauku ya Mpendwa kwa bibi-arusi wake (7:10). Mwimbaji anatamani urafiki huo unaopatikana katika fumbo la upendo wa Kristo na muungano na bibi arusi wake mpendwa (Efe. 5:32).
110
Made with FlippingBook Digital Publishing Software