Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
UNABII: MATARAJIO YA UJIO WA KRISTO Msingi wa Kristo uliwekwa kwa uthabiti katika Torati, matayarisho yalifanyika kwa maongozi ya kimungu katika Historia, na shauku ilionyeshwa kiroho katika Ushairi. Katika vitabu vya Unabii shauku hii ilipevuka na kuwa matarajio ya Kimasihi juu ya Kristo. Ingawa Torati ilitazama chini kwenye msingi, Historia ilitazama kwa nje katika matayarisho, Ushairi ulitazama juu katika matamanio, na vitabu vya unabii vilitazamia mbele. Torati ilitoa mwelekeo wa kiadili wa watu, Historia ikatoa mwelekeo wa kitaifa, Ushairi mwelekeo wa kiroho, na Unabii mwelekeo wa kiunabii. Vitabu kumi na saba vya unabii viko katika madaraja matatu: manabii wa kabla ya uhamisho (Isaya, Yeremia, Hosea hadi Sefania) ambao maonyo yao yalisemwa kabla ya anguko la mwisho la Yerusalemu (586 K.K.), vitabu vya kipindi cha uhamisho (Maombolezo, Ezekieli, Danieli) ambao matamanio yao wakati wa utumwa wa miaka sabini yalikuwa kwa ajili ya urejesho wa nchi yao, na manabii wa baada ya uhamisho (Hagai, Zekaria, Malaki), ambao himizo lao kwa mabaki waliorudishwa nyumbani lilikuwa ni kujenga upya taifa lililoanguka. Manabii hawa wote wanadhihirisha kwa pamoja matarajio ya Kristo, lakini kila mmoja anafanya hivyo kwa namna yake mwenyewe. Isaya Isaya alikuwa na matazamio mengi ya Kimasihi. Alimwona Kristo akiwa Bwana “aliye juu na aliyeinuliwa” (6:1), Mwana wa bikira (7:14), “Mungu Mwenye Nguvu” na “Mfalme wa Amani” (9:6), Mwana-Kondoo aliyepigwa (sura ya 53), Mpakwa Mafuta (Masihi) wa Bwana (61:1-), lakini zaidi ya yote, Kristo anaonekana kama Mtumishi anayeteseka (taz. sura ya 53-62).
111
Made with FlippingBook Digital Publishing Software