Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Yeremia Yeremia anamfananisha Kristo na “chemchemi ya maji ya uzima” (2:13), “zeri katika Gileadi” (8:22), Mchungaji mwema (23:4), kama Daudi Mfalme (30:9) “Chipukizi la haki” (23:5), na kama “BWANA ni haki yetu” (23:6). Maombolezo Maombolezo kinatoa picha za kinabii za Kristo kama Aliyeteswa na Bwana (1:12), aliyedharauliwa na adui zake (2:15-16), “dhihaka kwa watu” (3:14), aliyepigwa na kutukanwa (3:30), lakini nyuma ya hayo yote ni Kristo Nabii anayelia (rej. Mt. 23:37-). Ezekieli Ezekieli anamtazamia Kristo Mrejeshaji wa taifa (sura 37), Mchungaji wa kundi (34:23), Msafishaji wa taifa (36:24-), lakini zaidi ya yote anamwona Kristo kuwa Utukufu wa Mungu (rej. sura ya 1, 43). Daniel Danieli anamtabiri Kristo kuwa “jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono” (2:45), “Masihi [mtiwa-mafuta]” (9:26), “Mwana wa Adamu” (9:26) “Mwana wa Adam” (7:13), na “Mzee wa Siku” (7:22). Hosea Hosea anamwona Kristo kuwa Mwokozi wa pekee (13:4), Mwana wa Mungu (11:1), Yule anayewakomboa na mauti (13:14), lakini hasa Mpenzi mwenye huruma (11:4). Yoeli Yoeli alitabiri kwamba Kristo angemimina Roho wake (2:28), angehukumu mataifa (3:2, 12), na angekuwa “kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli” (3:16).

112

Made with FlippingBook Digital Publishing Software