Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Amosi Amosi anamfananisha Kristo kama “mwana wa pekee” (8:10), Yule ambaye atajenga upya “hema ya Daudi” (9:11), na Yeye ambaye ni Mkulima wa watu wake (9:13). Obadia Obadia anamwonyesha Kristo kama Bwana wa ufalme (mst. 21) na Mkombozi wa mabaki watakatifu (mst. 17). Yona Yona anatoa taswira ya Kristo kama Nabii wa mataifa (3:4), na yule aliyefufuka (1:17, taz.Mt. 12:40). Mika Mika alimtabiri Kristo kuwa “Mungu wa Yakobo” (4:2), Mwamuzi wa mataifa (4:3) na “mtawala katika Israeli” (5:2). Nahumu Nahumu anamwona Kristo kuwa “Mungu mwenye wivu” (1:2), Mlipiza kisasi kwa adui zake. Habakuki Habakuki alitoa taswira ya Kristo kama “Mtakatifu” (1:12), ambaye huwahesabia haki wenye haki kwa imani (2:4), na ambaye siku moja ataijaza dunia na “maarifa ya utukufu wa Bwana” (2:14). Sefania Sefania anamwona Kristo kama Bwana mwenye haki ndani ya Israeli (3:5), shahidi dhidi ya mataifa (3:8), na Mfalme wa Israeli, BWANA (3:15).

113

Made with FlippingBook Digital Publishing Software