Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Hagai Hagai anamwona Kristo kama Mrejeshaji wa utukufu wa hekalu (1:7 9), Mpinduaji wa falme (2:22), na “pete yenye muhuri” kwa Israeli (2:23). Zekaria Zekaria amejaa matarajio ya Kimasihi. Anamwona Kristo kuwa mtumishi wa Mungu “Aitwaye Chipukizi” (3:8), Mfalme mwenye ushindi (9:9), Mchungaji wa walio wanyonge kabisa (11:7), “Yeye ambaye walimchoma” (12:10), chemchemi ya maji ya utakaso (13:1), “Mfalme juu ya nchi yote” (14:9), na “Mfalme, BWANA wa majeshi” (14:17). Malaki Malaki anamtazamia Kristo kurudi kwenye hekalu lake akiwa “mjumbe wa agano” (3:1), “mfano wa moto wa mtu asafishaye” (3:2), na kama “jua la haki” lenye kuchomoza likiwa na uponyaji katika mbawa zake (4:2). Kila nabii alikuwa na seti yake mwenyewe ya mafumbo ya Kimasihi, lakini wote walishiriki tumaini moja la Kimasihi. Tarajio lao lilikuwa katika ujio wa Kristo, ambaye Musa alimwekea msingi, ambaye taifa lilikuwa limefanya matayarisho kwa ajili yake, na ambaye washairi walikuwa wamemtazamia kwa shauku. INJILI: KUDHIHIRISHWA KWA KRISTO Matarajio ya Agano la Kale ni utimilifu wa Agano Jipya. Agano la Kale linashughulika na maandalizi na matarajio ya kitaifa kwa ajili ya Kristo; Injili zinahusu udhihirisho wa Mwokozi katika mwili. Udhihirisho wake kama ulivyoandikwa katika Injili una sehemu nne. Jedwali ifuatayo inaonyesha udhihirisho huu wa Kristo, katika sitiari zake nyingi.
114
Made with FlippingBook Digital Publishing Software