Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

8. kutokana na wana wa Sulemani (1 Nya. 28:4-7) 9. angezaliwa na bikira (Isa. 7:14) 10. katika mji wa Bethlehemu (Mika 5:2) 11. takriban miaka 483 baada ya wakati wa Nehemia (444 K.K.; Dan. 9:25) 12. angepanda kama Mfalme kuingia Yerusalemu (Zek. 9:9) 13. angeteseka na kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu (Isa. 53, taz. Zab. 22) 14. lakini angefufuka katika wafu (Zab. 2, 16) Utimilifu wa Kanuni za Kimasihi Unabii mwingine, ambao si utabiri wa moja kwa moja, ulitumiwa kihalali katika Agano Jipya kwa habari ya Kristo kwa sababu ulijumuisha ukweli fulani katika maisha ya nabii au watu wa Masihi, ambao kwa sababu ya utume wao wa matayarisho katika Agano la Kale, wangeweza kupata utimilifu wake kamili katika nafsi ya Masihi Mwenyewe. Unabii kama huo hautajwi kuwa umetimizwa katika Agano Jipya kwa maana ya kutimia kwa utabiri fulani mahususi wa Kimasihi, bali katika maana ya kwamba kuna kanuni ya Kimasihi katika unabii huo ambayo imepata maana yake kikamilifu katika Kristo. Sasa, si jambo rahisi kila wakati kubainisha ni nini kinatabiri na nini kisichotabiri kwa sababu hakuna njia kamilifu na isiyokosea ya kung’amua utofauti huo. Kanuni iliyopendekezwa ni hii: ikiwa kifungu, katika muktadha wake wa Agano la Kale, kilikusudiwa na Mungu kutoa habari mapema juu ya kuja kwa Kristo, basi ni cha Kimasihi katika maana ya kutabiri (kwamba kimenukuliwa katika Agano Jipya au la). Kwa upande mwingine, ikiwa kifungu katika muktadha wake kinarejelea hasa hali ya

71

Made with FlippingBook Digital Publishing Software