Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
2. Unabii mwingine haukuwa utabiri wa moja kwa moja juu ya Kristo lakini Agano Jipya limeunukuu kwa kuuhusianisha naye kwa sababu kimsingi ulibeba kanuni ya Kimasihi . 3. Kulikuwa na “unabii” ambao haukuhusiana kabisa na Kristo wala kunukuliwa popote katika Agano Jipya, lakini kwa sababu unatoa “picha” ya kile ambacho Yesu alitimiza sawa sawa na vifungu ambavyo vilikuwa vya Kimasihi kimsingi, unaweza kutumika ipasavyo kwa habari ya Kristo. Hizi zinaitwa “picha za Kimasihi” ili kuzitofautisha na “kanuni za Kimasihi.” Pengine kuna aina ya nne ya unabii wa Kimasihi, yaani, utabiri lakini haukunukuliwa kuhusiana na Kristo katika Agano Jipya, kwa sababu hawakuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Labda “nyota ya Yakobo” katika Hes.
24:17 ni mfano wa aina hii ya unabii. Utimilifu wa Utabiri wa Kimasihi
Kwanza, kulikuwa na matukio mengi ambayo yalikuwa ni utimilifu wa utabiri wa moja kwa moja kuhusu Masihi au Mwokozi ajaye. Kwa mfano, ilitabiriwa kwamba Kristo:-
1. angezaliwa na mwanamke (Mwa. 3:15) 2. kupitia ukoo wa Shemu (Mwa. 9:26) 3. kutoka katika uzao wa Abrahamu (Mwa. 12:3; 15:5) 4. na kutoka katika uzao wa Isaka (Mwa. 21:12) 5. na kutoka katika uzao wa Yakobo (Mwa. 26:4)
6. kutoka kabila la Yuda (Mwa. 49:10) 7. wa ukoo wa Daudi (2 Sam. 7:12)
70
Made with FlippingBook Digital Publishing Software