Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
huu na maelezo yake yote kuwa ni mfano au kivuli cha upendo wa Kristo kwa Kanisa. Ingekuwa bora kuzingatia shairi hili la upendo kuwa kielelezo , badala ya unabii wa kitaipolojia wa Kristo. Bila kujalisha mtu anazipa hadhi gani “picha” hizi za Kristo katika Agano la Kale, iwe ni unabii wa kitaipolojia (mfano) au kielelezo, ni lazima ikubalike kwamba picha za Agano la Kale hazitoi taswira inayofanana kwa kiwango kikubwa na uhalisi wa mtu (mhusika halisi) ndani ya Agano Jipya. Agano la Kale linatoa picha nyingi za Kristo; ni aina fulani ya albamu ya picha za Kimasihi, lakini Agano Jipya linamfunua Kristo halisi aliyewakilishwa na picha hizo. KRISTO: KUTABIRIWA KATIKA A.K NA UTIMILIFU KATIKA A.J Kuna namna ya tatu ambayo maagano haya mawili yanahusiana, yaani kwa msingi wa yaliyotabiriwa kuhusu Kristo hadi yale yanayotimilizwa katika Kristo. Huu, bila shaka, ndio umuhimu wa unabii wa Kimasihi. Kulikuwa na ahadi nyingi za Kimasihi kutoka Mwanzo (3:15) hadi Malaki (4:2), ambazo baadhi yake zimejadiliwa tayari (sura ya 2). Kutoka Unabii hadi Historia Agano Jipya linahusiana na la Kale jinsi historia inavyohusiana na unabii wake. Sasa kulikuwa na matamko mengi ya “utabiri” yaliyotolewa juu ya Kristo katika Agano la Kale, baadhi yakiwa wazi zaidi kuliko mengine. Matamko haya ya kinabii ya Agano la Kale yanaweza kutazamwa kuwa yametimizwa katika Kristo kwa angalau njia tatu tofauti: 1. Baadhi ya unabii ulikuwa utabiri wa moja kwa moja kuhusu
Kristo na kwa sababu hiyo unaweza kuhusishwa na Yeye kihalali, kama Agano Jipya linavyofanya kwa kawaida.
69
Made with FlippingBook Digital Publishing Software