Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
• Sulemani na hekima yake (Mt. 12:42) • “Mwamba” nyikani (1Kor. 10:4) • “Mana” kutoka mbinguni (Yh 6:41) • “Nyoka” jangwani (Yh 3:14)
Ni vigumu kuweka mipaka upande huu wa dhana ya kidini kuhusiana na picha za Kristo katika Agano la Kale ambazo Agano Jipya halijazitumia katika msingi huo. Kwa upande mwingine, kama ilivyo kwa taipolojia , ingeonekana kuwa ufinyu wa fikra sana kuweka “picha” za Kristo ndani ya boksi la mambo yale tu ya Agano la Kale ambayo Agano Jipya linayahusianisha na Kristo. Ingekuwa bora zaidi kutumia kanuni ya jumla inayohusika katika orodha iliyo hapo juu, yaani kwamba kitu chochote ambacho kinaakisi ipasavyo kipengele fulani muhimu cha utume wa Kimasihi wa Kristo na ambacho kina sitiari za Kimasihi zinazoendana nacho katika Biblia. Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazosadikika kuwa vielelezo vya Kristo katika Agano la Kale: • Safina ya Nuhu ya usalama (Mwa 7; taz. 1 Pet 3:21) • Isaka, dhabihu (Mwa. 22; taz. Yh. 3:16, Ebr. 11:19) • Ngazi ya Yakobo kutoka duniani hadi mbinguni (Mwa 28; taz. Yh. 1:51; 14:6) • Yusufu, kukataliwa na ndugu zake (Mwa 37; taz. Yh. 1:10-11) • Miji ya makimbilio (Kum. 4, 19; taz. 1 Pet 5:7; Mt. 11:28) • Mkombozi wa jamaa (Rut 4; taz. Gal. 3:13) • Mpendwa, n.k. (Wim; taz. Efe. 5:25) Kuna picha nyingi nzuri za Kristo katika Wimbo Ulio Bora, kama vile “Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi” (5:10), “dhahabu safi sana” (5:11), na “mzuri sana” (5:16). Hata hivyo, dhana za kidini zilizoongezwa kwenye taipolojia na mafumbo yaliyokithiri mara nyingi sana zimechukulia wimbo
68
Made with FlippingBook Digital Publishing Software