Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Kristo katika Picha na katika Mwili Kuna picha nyingi za Kristo zinazofaa katika Agano la Kale ambazo, tukisema vizuri, hazipaswi kuainishwa kama mifano. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa kama “aina” ( typos ), ambalo kwa kawaida hutafsiriwa kama “mfano” au “kielelezo” (1 Tim. 4:12), halina maana ya kiufundi (istilahi) katika Agano Jipya na linatumika kuhusiana na Kristo mara moja tu (Rum. 5:14), ambapo Adamu anasemekana kwamba alikuwa “mfano” wa Kristo. Kile kinachomaanishwa na neno “mfano” wa Kristo wakati mwingine huitwa “kivuli” au “nakala” ( hypodeigma ) (Ebr. 8:5; 9:23) na wakati mwingine hata “fumbo” ( parabole ) (Ebr. 9:9) na hata ufananisho au “nakala” ( antitypos ) (Ebr. 9:24). Maneno haya yana maana mbalimbali ikiwa ni pamoja na “michoro ya misumari” (Yh. 20:25), “onyo” (1Kor. 10:11), au “umbo” (sanamu) (Mdo. 7:43) na kwa sababu hiyo maana ya neno “mfano” haiwezi kuamuliwa kutokana na matumizi ya Agano Jipya. Kwa msingi wa kanuni ya jumla ya ufasiri, ingeonekana kuwa bora kutumia maana ya mfano kwa ajili ya kurejea watu, taasisi na ibada za Agano la Kale ambazo ziliwekwa awali na Mungu kuwa vivuli vya kile ambacho Kristo angekuja kutimiliza baadaye. Kila kitu kingine ambacho kinaweza kutumika katika mantiki hii kwa habari ya Kristo (kwamba Agano Jipya linakitumia hivyo au la) basi kitaitwa picha au kielelezo cha Kristo. Mfano haukutoa tu picha au taswira ya Kristo bali ulikuwa ni aina ya unabii wa wazi kwamba Kristo angetimiliza kazi ya mfano husika. Ndivyo ilivyokuwa kuhusu dhabihu, hekalu, ukuhani, na sikukuu za Agano la Kale. Vilikuwa vivuli vya muda ambavyo vilielekeza kwenye ukamilifu wake katika Kristo. Lakini, zaidi ya mifano hii, kuna picha nyingi katika Agano la Kale ambazo zinatumika ipasavyo kama vielelezo vya Kristo. Baadhi ya picha hizo, Agano Jipya linazihusianisha na Kristo na zingine hazijatajwa kabisa katika A.J. Katika kundi la zile zilizonukuliwa ni: • Siku tatu za Yona mchana na usiku ndani ya nyangumi (Mt. 12:40)

67

Made with FlippingBook Digital Publishing Software