Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

milele (9:15), agano la milele (13). 20). Udumifu huu wote ni kwa sababu Kristo ndiye Kuhani Mkuu anayetimiliza mfumo wa Walawi, ana kiti cha enzi (1:8), ukuhani (5:6; 7:20), neno la kiapo (7:28), na utukufu (13:21) ambavyo vyadumu milele . Kutoka Kaida za Kiibada hadi Uhalisi Kile ambacho kimesemwa kuhusu ukuhani, dhabihu na hekalu la Agano la Kale kinaweza pia kusemwa kuhusu Sabato na sikukuu. “Mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili [uhalisi] ni wa Kristo.” (Kol. 2:17). Mara uhalisi unapokuwa umefika, kaida ambayo ilitangulia haihitajiki tena. Kwa maneno mengine, vivuli vya Agano la Kale vinatimizwa katika kweli ya Agano Jipya. Kwa kuwa sura iliyotangulia imejadili kuhusu tafsiri ya sikukuu za A.K katika msingi wa Kristo, itatosha hapa kusema kwamba Kristo ametimiliza na kuvuka taratibu za Walawi za Agano la Kale kama ambavyo mtu ni zaidi ya kivuli chake mwenyewe wakati wa mchana. Ni wakati tu nuru ya kinabii ilipochomoza ndipo vivuli vya Kristo vilikuwa virefu. Baada ya mwanga kamili kuja, vivuli vilitoweka. Hoja ya Paulo katika Wakolosai ilikuwa ni kwa ajili ya kufutwa, katika Kristo, kwa kaida zote za kiibada za Agano la Kale zilizotenganisha waamini. Kristo ameifuta “ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani” (Kol. 2:14). Paulo aliuliza, “kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse.... hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili” (Kol. 2:20-23). Mwamini wa Agano Jipya amekufa kwa habari ya matakwa ya sheria (3:2) na ameinuliwa juu ya taratibu hizi hata kuufikia uhalisi mpya katika Kristo na, kwa sababu hiyo, anapaswa “kutafuta yaliyo juu” (3:1).

66

Made with FlippingBook Digital Publishing Software