Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
• Malaika (1:4) • Tumaini la Agano la Kale (7:19)
• Agano la kale (7:22) • Ahadi za kale (8:6) • Dhabihu za Agano la Kale (9:23) • Nchi yao ya kidunia (tumaini na hatima) (11:16) • Mali za zamani (10:34) • Ufufuo wa Agano la Kale (11:35)
Na kwa sababu ya mambo hayo, mwandishi wa Waebrania asema, “… tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi , na yaliyo na wokovu,” (6:9) kwa sababu “Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora , ili wao [waamini wa A.K] wasikamilishwe pasipo sisi” (11:40). Kwa hiyo, kivuli cha mambo ya Kale lazima kitoe nafasi kwa uhalisi mkamilifu na wa kudumu katika Kristo. Ni kwa sababu hii waraka kwa Waebrania unasema juu ya sifa isiyo ya kudumu ya: • Ukuhani wa Haruni—ambao ulihitaji “mabadiliko” (7:12). • Makuhani wa ukoo wa Haruni—ambao “wanatumikia mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni” (8:5). • Sheria—ambayo pia ilikuwa ni “lazima ibadilike” (7:12). • Hema—ambayo ilikuwa “mfano” tu wa ile halisi (8:5) • Dhabihu—ambazo “zilifutwa” (10:9). • Agano la kale—ambalo halikuwa “bila upungufu” (8:7) na hivyo ni “kuukuu” na li “karibu na kutoweka” (8:13). Na kwa kuwa kivuli cha agano la kale kilikuwa cha muda tu, uhalisi wa agano jipya lazima uwe wa mwisho ili kukomesha lile la kale. Kwa hiyo kitabu cha Waebrania kinasema juu ya wokovu wa milele (5:9), hukumu ya milele (6:2), ukombozi wa milele (9:12), Roho wa milele (9:14), urithi wa
65
Made with FlippingBook Digital Publishing Software