Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

unifanyie” hadi kwenye kiwango cha juu zaidi cha “Nakupenda kwa sababu Mungu alinipenda kwanza,” basi upendo unaweza kukamilishwa na hofu ikatupwa nje. Kwa maana ikiwa mtu ana upendo huu mkamilifu, hafanyi kazi tena kwenye viwango vya matokeo yanayofanana bali kwenye uwanda wa vigezo vya kimungu. Kama vile Yohana alivyosema, “Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana” (1 Yh 4:11) au, tena, “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu” (1 Yh 3:16). Kwa hivyo, Agano la Kale na Agano Jipya zimeunganishwa kwa njia isiyoweza kutenganishwa katika dhana ya maadili ya upendo. Lakini kanuni ya upendo wa kubadilishana katika Agano la Kale inakamilishwa katika upendo wa kujidhabihu ambao Yesu alionyesha katika Agano Jipya. Kuna uhusiano mwingine baina ya A.K na A.J. Huu unapatikana katika uhusiano kati ya mfano [kivuli] na uhalisi : kati ya vivuli vya Kristo katika Agano la Kale na uhalisi wa Kristo katika Agano Jipya. Kutoka Kivuli hadi Utimilifu Kitabu cha Waebrania kinakazia uhusiano huu kati ya ukuhani wa Walawi na ule wa Kristo. Tunasoma, “Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe.” (Ebr. 10:1, NMM). Yaani, taratibu za Agano la Kale zilisimama kama vivuli tu vya yale ambayo Kristo mwenyewe alikuja kutimiza (taz. sura ya 2). Hii ndiyo sababu waraka kwa Waebrania unawasilisha kiini au uhalisi wa kweli wa Kristo kuwa bora kuliko : KRISTO: KUTOKA VIVULI VYA AGANO LA KALE HADI UHALISI KATIKA AGANO JIPYA

64

Made with FlippingBook Digital Publishing Software