Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

wameficha maana ya amri hii kwa kuuliza, “Na jirani yangu ni nani?” (Lk 10:29). Yesu alijibu kwa kusimulia hadithi ya Msamaria mwema, ambaye alijithibitisha kuwa “ jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi” (10:36). Kwa maneno mengine, Yesu alionyesha kwamba wanadamu wasijaribu kukwepa kuwapenda wengine kama wanavyojipenda wenyewe kwa kupunguza fasili ya neno jirani wakitaka kumaanisha kwamba mtu hapaswi kuwapenda wale ambao si jirani zake. Lakini Yesu hakuleta tu maana ya kweli ya torati katika suala la upendo, pia alitimiza au kukamilisha maana ya torati kwa kuuweka upendo kwenye kiwango cha juu zaidi. Torati ilisema wapende wengine kama nafsi yako; kupitia kifo chake Yesu alionyesha kwamba mtu anaweza kuwapenda wengine kuliko nafsi yake. “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yh 15:13). Na “Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ….kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu” (1 Yh 4:17). Kwa hiyo maagizo ya Agano la Kale kuhusu upendo hayajathibitishwa tu na Yesu bali yanavukwa katika viwango vya upendo mkamilifu wa Agano Jipya. Sheria ya Agano la Kale ilikuwa na adhabu zilizoambatana nayo, jambo ambalo lilipelekea hofu ya matokeo ya kutotii. Dhana ya upendo ya Agano Jipya inainua na kukuza msukumo wa upendo na kwa hiyo inaondoa hitaji la hofu. “Kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo” (1 Yh 4:18). Baada ya Yesu kuonyesha, kupitia mafundisho na maisha yake na kifo chake kwa ajili ya wenye dhambi , kwamba mtu anapaswa kuwapenda wengine zaidi ya nafsi yake, na si tu kama anavyojipenda mwenyewe, upendo uliinuliwa kutoka kiwango cha maadili ya asili au ya upatanifu, kulipa fadhila na kutendeana kwa kiwango kile tunachotendewa, hadi kufikia kiwango kisicho cha kawaida – yaani maadili ya kidhabihu. Yaani baada ya upendo kuinuliwa kutoka katika kiwango cha “Nakupenda kwa sababu hivi ndivyo nataka

63

Made with FlippingBook Digital Publishing Software