Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu ?” (Mt 19:3). Kwa vile “ridhaa” ya Musa ilipotoshwa na kuchukuliwa kama “amri” ya Mungu, Yesu alithibitisha fundisho la kweli la Agano la Kale kuhusu ndoa kwa kusema, “lakini tangu mwanzo haikuwa hivi” (Mt. 19:8). Agano la Kale lilikuwa kinyume cha talaka kwa sababu Mungu alikuwa amewaunganisha mume na mke katika muungano mtakatifu (Mat. 19:5). Malaki anamnukuu Bwana akisema, “Nakuchukia kuachana .... basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana” (2:16). Kwa hiyo ukweli wa maadili kuhusu ndoa uliomo katika Agano la Kale, lakini umefichwa na mapokeo, unathibitishwa tena na kufafanuliwa kikamilifu zaidi na Kristo katika Agano Jipya. Kristo alithibitisha ubora wa sheria kwa kuleta maana yake iliyokusudiwa na Mungu. Maagizo ya Agano la Kale Yanaletwa kwenye Ukamilifu katika Agano Jipya Si tu kwamba Yesu alithibitisha maana ya kweli ya maadili ya Agano la Kale, bali aliivuka . Kulingana na Yesu, kiini cha kweli cha maadili ya Agano la Kale ni “kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na ... jirani yako kama nafsi yako,” kwa kuwa “katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii” (Mt. 22:37, 39-40). Sasa ukweli huu kwa hakika umo katika Agano la Kale, lakini umefafanuliwa kwa ukamilifu zaidi katika Agano Jipya. Kwa mfano, ubao mzima wa pili wa amri unadokeza kwamba mtu anapaswa kuzingatia maslahi na ustawi wa mwingine moyoni mwake (rej. Kut. 20:12-17). Kulikuwa na kanuni za jinsi ya kuwatendea watumishi (Kut. 21), heshima ambayo ni lazima kuwa nayo kwa mali ya jirani (Kut. 22), na upendo kwa adui za mtu (Kut. 23, taz. Yona 4:10-11), na hata upendo na heshima kwa wale walio wa hali ya chini kabisa katika jamii (rej. Hosea 3:1-). Upendo ulijumuishwa ndani ya Agano la Kale, lakini ulifafanuliwa kikamilifu zaidi katika Agano Jipya. Wayahudi wa siku za Yesu walikuwa

62

Made with FlippingBook Digital Publishing Software