Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Sababu ya Watu Mara Nyingi Kushindwa Kumwona Kristo katika Agano la Kale
Hata hivyo, kwa juu juu, haiko wazi sana kwamba Kristo ndiye mada ya Agano zima la Kale. Kwa kweli, Kristo amefichwa katika Agano la Kale. Ukweli kwamba Kristo haonekani dhahiri katika kurasa za Agano la Kale unaweza kushuhudiwa na Wayahudi na Wakristo kadhalika. Ingawa Wayahudi wengi wanashindwa kumpata Kristo katika Agano la Kale kwa sababu ya upofu wa Torati (2 Kor. 3:14-16), Wakristo wengi wanashindwa kumwona Kristo katika Agano la Kale kwa sababu tu ya kutojua maandiko. Kuhusu kushindwa kwa Wayahudi kumwona Yesu katika Maandiko yao, Paulo aliandika hivi: “ila fikira zao zilitiwa uzito.... Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa” (2Kor. 3:14, 16). Wakristo akili zao zimefunguliwa wapate kumfahamu Kristo na hawapaswi kuwa na shida ya kumwona akiwa amefichwa katika maagizo ya Agano la Kale. Licha ya ukweli huu, Yesu alilazimika kuwaambia wanafunzi wake wawili, “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! .... Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza [akawafasiria] katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” (Lk 24:25, 27). Na baadaye, kwa wanafunzi wengine, “akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko” (Lk 24:45). Kristo alifichwa katika Agano la Kale, lakini hili lilidhihirishwa baadaye kwa wanafunzi katika Agano Jipya. A.J. limejumuishwa katika la Kale na A.K. limefafanuliwa katika Jipya Ukweli wa maagano haya mawili unahusiana kimaadili, kwa maana Agano Jipya linafafanua maagizo ambayo Agano la Kale limeyajumuisha . Kwa mfano, Agano la Kale lilikuwa limefundisha kudumu kwa ndoa ambayo, kwa sababu watu walikuwa wameipotosha, Musa aliruhusu watu kuivunja (Kum. 24:1-4). Kwa msingi huu “Basi Mafarisayo wakamwendea,
61
Made with FlippingBook Digital Publishing Software